Huku
Ghana na Senegal zikichuana katika mechi ya leo kundi la C,Wachezaji
wawili muhimu katikja mechi hiyo huenda wasicheze kiputo hicho
kinachongojewa kwa hamu na gamu
Nahodha wa timu ya Ghana Asamoah
Gyan anaugua maradhi yanayosemekana kuwa ni malaria huku Mshambuliaji wa
Senegal Diafra Sakho akidaiwa kuugua maumivu ya mgongo.Vilevile Timu
hiyo ya Senegal huenda ikamkosa mchezaji Sadio Mane wa kilabu ya
Southampton ambaye anauguza jereha.
Diafra Sakho akiifungia kilabu yake ya West Ham
Shirikisho la soka la Ghana
limetoa maelezo kuwa Gyan alikuwa amepumzishwa hospitali katika mji wa
Mongomo tangu Jumamosi jioni na kuruhusiwa Jumapili asubuhi ,na
inaelezwa kuwa maradhi hayo yametibiwa katika hatua za awali na mchezaji
huyo anaendelea vyema.
Kukosekana kwa Gyan katika kikosi cha
taifa lake, kunaweza kuwa mtihani kwa kocha wake mpya wa Ghana Avram
Grant aliyewahi kuwa boss wa Chelsea ambaye lengo lake ni kuona Black
Stars inapata ushindi dhidi ya Senegal.
Lakini walau analo chaguo,
anaweza kumwita mchezaji wa timu ya Marseille ,mchezaji wa mbele Andre
Ayew na pia mchezaji wa timua ya Everton Christian Atsu ama hata Mubarak
Wakaso wa timu ya Celtic.
Post a Comment