Chama cha Mapinduzi (CCM) wiki ijayo kitaanza rasmi vikao vyake kwa
ngazi ya Taifa vitakavyo chunguza maadili ya viongozi ikiwa ni
maandalizi ya kuwapata wagombea wanaokubalika na wananchi katika
Uchaguzi Mkuu ujao.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alitoa taarifa hiyo jana
katika mkutano maalumu wa kuwashukuru Watanzania kwa kukichagua chama
hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 14, mwaka
jana. Alisema chama chake kinajipanga kuwa na viongozi wasio
wamangimeza na wenye moyo wa kuwatumikia wananchi.
Katibu huyo Mkuu aliwashukuru Watanzania kwa kukipa ushindi chama
chake na kubainisha kuwa kitaifa, CCM imeshinda kwa asilimia 81.
Hata hivyo, alisema katika maeneo ambayo imeshindwa kama Wilaya ya
Pangani, itafanyika tathmini na watajipanga kuhakikisha Uchaguzi Mkuu
ujao wanapa ushindi wa kishindo.Alisema watahakikisha wanashinda katika
maeneo yote waliyofanya vibaya.
Post a Comment