Mawakala zaidi ya watano wamejitokeza kwa Klabu
ya Simba na kuomba kumchukua kiungo wa klabu hiyo, Said Ndemla kwenda kufanya
majaribio katika moja za timu za nje, hasa barani Ulaya.
Ikiwa mipango hiyo itakubalika na kwenda
inavyotakiwa, maana yake ni kuwa itakuwa mara yake ya kwanza.
Awali, kulitolewa taarifa kuwa, wachezaji
wengine wa klabu hiyo, Ramadhani Singano‘Messi’ na Hassan Kessy, walikuwa
kwenye mipango ya kwenda kufanya majaribio katika Klabu ya Real Madrid ya
Hispania.
Evans Aveva ambaye ni rais wa Simba ndiye
aliyefunguka kila kitu kwa kusema:“Tunashukuru tunaendelea kutengeneza vijana na
wanafanya vizuri, mawakala watano kutoka nje wameanza kuvutiwa na uwezo wa Said
Ndemla, mipango inafanyika ili baada ya msimu huu wa ligi kuu kumalizika aweze
kwenda nchi tofauti kufanya majaribio.
“Kwenye mchezo wetu na Azam viongozi wa Real Madrid walivutiwa na kiwango cha Singano na Kessy, waliomba CD zao kwenda kuifanyia kazi.
“Ni jambo la kujivunia, zaidi mashabiki wetu waendelee kuisapoti na kuiunga timu mkono ili kuweza kusonga mbele na kufanya vizuri, wasikate tamaa, timu itafanya vema.”
Post a Comment