Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya Kilwa mkoani Lindi Ali Mtopa akizungumza na
mwaandishi wa habari wa gazeti la raia Tanzania
mwaandishi wetu
Kilwa......Wazazi na walezi
Mikoa ya Lindi na wametakiwa kuwasimamia watoto wao kielimu
ili kuepuka kugeuzwa vibarua wa kufanya kazi
ngumu wakati wa uchimbaji wa gesi utakapoanza.
Ushauri huo umetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kilwa
na mwenyeki wa chama cha mapinduzi mkoa wa Lindi Ali Mtopa wakati
alipokuwa anazungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea ofisi kwake
jana
Mtopa alisema wazazi wana wajibu mkubwa kuwasomesha vijana wao
kwenda sambamba na mabadiliko ya kimaendeleo na fursa zinazo jitokeza katika
mikoa ya kusini Lindi na Mtwara ambazo zinahitaji watu waliosoma.
Alisema uchimbaji wa gesi na mafuta, unahitaji kuwa na wafanyakazi
waliosoma kama watoto hawatasomeshwa kikamilifu wataishia kufanya kazi ya
kubeba mizigo na vibarua kwa ujira mdogo.
“nawaomba wazazi wezangu tuwasimamie watoto wetu ili wasome
vizuri,na tuache tabia ya kuwaoza umri mdogo tutawafanya kuwa vibarua” alisema
Mtopa
Mtopa alisema kutokana na historia ya mikoa ya kusini hali ya
kimaendeleo iko nyuma iliyosababishwa na ukosefu wa elimu hivyo ni
jukumu la wazazi kusimamia elimu ya watoto ikiwa ni pamoja na kuhakikisha
wanakwenda shule kwa wakati.
“Elimu ni msingi wa kila kitu na ukiwa na elimu
utaweza kuepuka na matatizo ya ujinga ,maradhi na umaskini”. Alisema Mtopa.
Post a Comment