Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na
wananchi wa kijiji cha Surubu, Kata ya Komaswa wakati wa ziara yake
wilayani Tarime Mkoa wa Mara.Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewataka wananchi wa
vijiji vya wilayani hapa kutoa taarifa za mianya ya rushwa wakati
wanapoomba kuunganishiwa umeme majumbani.Muhongo
alisema hayo juzi alipokuwa akikagua awamu ya pili ya Mradi wa Umeme
Vijijini unaoendelea kwa nchi nzima na ambao mkoani Mara unatekelezwa
katika vijiji 197.Alisema
katika mradi huo, Serikali haitamwonea huruma mfanyakazi yeyote wa
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) atakayebainika kuomba rushwa ili
atoe huduma.
“Msitoe
hongo,” alisema Profesa Muhongo. “Kati ya vitu ambavyo Serikali haitaki
kuvisikia ni rushwa. Msidanganywe kuwa mkitoa rushwa ndiyo
mtarahisishiwa kupata umeme kwa haraka.”
Alisema
gharama zote za kuunganishiwa umeme kwa mwanakijiji zinalipwa na
Serikali na kiasi cha Sh27,000 ni tozo ya Kodi ya Ongezeko la Thamani
(Vat).
Baadhi ya
watu walilalamika kuwa mradi huo unawanufaisha wakazi wachache walio
jirani na barabara zinakopita nguzo za umeme na kuacha maeneo yaliyo na
watu wengi na huduma za kijamii kama shule na zahanati.
“Huduma
inayotolewa na ofisi za Tanesco katika wilaya hii ni mbovu sana na mradi
huu unapita mbali na makazi ya wanakijiji wengi. Tunaomba utusaidie ili
tupate huduma bora,” alisema mkazi wa Bunda, Sherida Charles.
Naye
kaimu mkuu wa wilaya hiyo, Angelina Mabula aliwataka wananchi
kuchangamkia fursa hiyo ya kuunganishiwa umeme ambayo alisema ni chachu
ya maendeleo katika sekta mbalimbali hasa ya afya na elimu.
“Hivi sasa kuna ujenzi wa maabara za kisasa katika shule zetu, haziwezi kufanya kazi bila umeme,” alisema Mabula.
Mabula
alisema vikiunganishiwa umeme, vituo vya afya vitaondokana na adha ya
wauguzi kuhangaika na vibatari wanapotoa huduma, hususan kwa wajawazito.
“Watakuwa
pia wamejikomboa kutembea umbali mrefu kutafuta huduma bora na salama
na hakutakuwa na haja ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo,”
alisema Mabula.
Aidha
aliwataka wananchi kulinda miundombinu ya umeme hasa wale walio zoea
kuiba mafuta ya Transifoma na nyaya kwa makusudi ya kuuhujumu uchumi
wananchi
chanzo:gazeti la mwananchi
Ndugu Wanaotafuta Mkopo
ReplyDeleteWewe katika matatizo yoyote ya fedha? Je, unataka kuanza biashara yako mwenyewe? Hii kampuni ya mkopo ilianzishwa Mashirika ya haki za binadamu duniani kote kwa madhumuni ya kusaidia maskini na watu wenye matatizo ya kifedha ya maisha. Kama unataka kuomba mkopo, kupata nyuma sisi na maelezo hapa chini ya barua pepe: elenanino0007@gmail.com
jina:
kiasi mkopo inahitajika:
Mkopo Muda:
Namba ya simu ya mkononi:
Asante na Mungu awabariki
kujiamini
Bi Elena