Pallangyo kwa sasa anakua Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita.
Rais Kikwete amefanya uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa.
Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya Jumatano, Novemba 5,
2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa
walioteuliwa ni pamoja na Dkt. Donan Mmbando ambaye anakuwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuchukua nafasi ya Pallangyo.
Katika uteuzi huo Dkt. Yohana Budeba anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mbogo Futakamba kuwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Maji na Dkt. Adelhelm James Meru ambaye anakuwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Utalii na Maliasili.
Kabla ya uteuzi wake, Dkt Mmbando alikuwa Mganga Mkuu wa Serikali,
Dkt. Budeba alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na
Mifugo, Mhandisi Futakamba alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na
Dkt. Meru alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya
Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).
Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete amemhamisha Bibi
Maimuna Tarishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria,Adoh Steven Mapunda, Mkurugenzi
Mtendaji, Manispaa ya Bukoba amepanda na kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa
Arusha, Severine Kahitwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita anakuwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro na Dkt. Faisal Issa, Katibu Tawala wa Mkoa
wa Kilimanjaro anahamishiwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Kanali (Mst) Joseph
Simbakalia, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa EPZA
kuchukua nafasi ya Dkt. Meru.
Uteuzi huo unaanza leo na Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa
Mikoa wameapishwa leo Alhamisi,Novemba 6, 2014, Ikulu, Dar es Salaam.
Post a Comment