0
Baadhi ya wabunge wameendelea kuishinikiza serikali kuwasilisha taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ili kubaini  ufisadi wa zaidi ya shilingi Bilioni 200 uliofanywa na baadhi ya vigogo kwenye akaunti ya Escrow kwa lengo la kuwezesha kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.
Wakichangia mapendekezo ya utekelezaji wa mpango wa taifa kwa mwaka 2015/16 Mbunge wa kigoma kusini Mhe. David Kafulila amesema haiwezekani familia chache zitafune fedha za umma,huku wengine wakitaka serikali kusema Ripoti hiyo itapatikana lini.
 
Mjumbe wa kamati ya bajeti ambae pia mbunge wa viti maalum Mhe.Christina Lissu amesema  taarifa iliyoletwa imeonyesha wafadhili hao wametoa kiasi kidogo cha fedha kutokana na kusubiri ripoti ya ukaguzi wa sakata la Escrow. 
 
Awali katika kipindi cha maswali na majibu kwa waziri mkuu,waziri Mkuu Mhe. Mizengo pinda amesema hajapokea taaarifa toka kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na kusikitishwa na maamuzi ya wahisani ya kusitisha kutoa fedha kusuburi Ripoti hiyo ambapo amehoji kikundi cha watu wachache watakaobanika kwenye Ripoti hiyo kuweza kusababisha nchi nzima kukosa kutekeleza Miradi ya Maendeleo.ITV

Post a Comment

 
Top