
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasiliana na baadhi ya wananchi waliokuwa
wakimjulia hali kupitia simu yake ya mkononi kupitia ujumbe mfupi(sms)
leo Jumatatu.Rais Kikwete anayepata matibabu katika hospitali ya Johns
Hopkins jijini Baltimore Maryland nchini Marekani anaendelea vizuri na
anafanya mazoezi mara kwa mara na afya yake inaendelea kuimarika
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
jana, Jumatatu, Novemba 10, 2014, alianza kuwasiliana na mamia kwa mamia
ya wananchi mbali mbali nchini kujibu ujumbe mfupi wa maandishi (SMS)
wa kumpa pole, kumtakia heri na nafuu ya haraka ambao amekuwa anatumiwa
na wananchi tokea mwishoni mwa wiki.
Tangu
alipofanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) Jumamosi iliyopita
kwenye Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore, Jimbo la Maryland,
Marekani, Rais Kikwete amepokea mamia kwa mamia ya SMS zikimpa pole na
kumtakia nafuu ya haraka.
Rais
Kikwete bado anaendelea kujibu SMS hizo na wananchi ambao wamemtumia
SMS Rais Kikwete waendelee kusubiri majibu ya Mhe. Rais kwa sababu
anakusudia kujibu SMS zote ambazo ametumiwa.
Aidha,
Rais Kikwete jana alizungumza kwa simu na uongozi wa juu wa Tanzania
kwa mara ya kwanza tokea afanyiwe upasuaji. Rais alizungumza na Makamu
wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda.
Wakati
huo huo, madaktari wanaondelea kumtibu Rais Kikwete jana waliondoa
bandeji kwenye sehemu ambako alifanyiwa upasuaji wakieleza kuwa hali
yake inaendelea vizuri na anapata nafuu kwa kasi nzuri.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
11 Novemba,2014
Post a Comment