Jengo la mashine ya kupampu maji
Mkuu wa wilaya ya Liwale mh.Ephraim Mmbaga alifanya ziara wiki iliyopita tarehe 2/11/2014 ya kukagua shughuli za kimaendeleo katika kijiji cha Mpigamiti kata ya Mpigamiti,akiwa ameongozana na diwani wa kata hiyo bwana Manjanjagara,diwani wa viti maalum Amina Mnoche pamoja na mfanyakazi kutoka idara ya maji alitembelea mradi wa maji uliojengwa na serkali ikishirikiana na Benki ya dunia na amewataka wananchi kuutunza vizuri mradi huo na kuyatumia maji hayo katika shughuli zao za kujiongezea kipato.
Mkuu wa wilaya mh.Ephraim Mmbaga akiangalia mashine ya kupampu maji
Katika ziara hiyo amepokea kero mbalimbali kutoka kwa wananchi na amewahidi kuzitafutia ufumbuzi haraka iwezekanavyo pia amewasisitiza wananchi kulima mazao ya aina mbalimbali ambayo yanayositawi vizuri kama alizeti, kunde aina ya mbaazi,viazi vitamu na maharage,kwani mazao hayo husitawi vizuri sana kutokana na ardhi ya kijiji hicho cha Mpigamiti kuliko kutegemea zao moja la korosho ambalo muda mwingine soko lake halina huhakika na malipo yake huwa unapokea nusu nusu.

Post a Comment