0
Serikali wilayani Hanang mkoa wa Manyara imeagiza kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria zaidi ya viongozi 8 wa serikali ya kijiji cha Gidika pamoja na mtendaji wa kata ya Getanusi kwa wilayani hanang kwa kusababisha mgogoro wa zaidi ya miaka mitano kutokana na kukiuka maazimio ya mkutano mkuu wa kijiji hicho juu ya ugawaji wa ardhi kwa wananchi wa eneo hilo.

Na hivi ndivyo maagizo hayo yanavyotolewa na mkuu huyu wa wilaya ya hanang Sara Msafiri huku kaimu afisa ardhi wilaya hapa akifafanua juu ya utaratibu wa eneo hilo ambalo limetolewa na serikali kwa wananchi kugawiwa katika kata hii ya Getanus baada ya shamba hilo kurejeshwa kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya shamba lililokuwa chini

Baada ya maagizo hayo ikiwemo kurejeshwa maeneo yaliyouzwa kinyume cha taratibu pamoja na yale ambayo viongozi walijigawia kinyume na mkutano mkuu wananchi wakapasa sauti zao kabla ya kuanza ugawaji huo upya.

Na huyu ni mmoja ya washukiwa wanaodaiwa kusababisha mgogoro huo kipindi cha uongozi wake.

Aidha inadaiwa wananchi wa kata hii kutoa vitisho vya kuwapiga mishale viongozi wa kijiji pamoja na wataalam wa upimaji wa ardhi pindi wanapojaribu kuendesha zoezi la upimaji katika eneo hilo.

Post a Comment

 
Top