Bohari ya
Dawa nchini Tanzania, MSD imeripotiwa kuwa imesitisha utoaji wa dawa
muhimu kwa taasisi za afya za serikali hadi hapo deni la shilingi
bilioni 90 linalodaiwa na wakala huyo litakapolipwa na taasisi hizo.
Sikika ambalo ni shirika lisilo la kiserikali linalohimiza huduma bora
za afya nchini Tanzania limeeleza Jumapili kwamba kiasi kikubwa cha
fedha kinachodaiwa na MSD kime mamlaka hiyo ya usambazaji dawa kushindwa
kununua dawa kwa ajili ya zahanati, vituo vya afya na taasisi nyingine
za tiba nchini kote.Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, Irenei Kiria amesema shirika lake lina taarifa rasmi kwamba MSD inaweza kutoa dawa na vifaa vingine vya tiba pale madeni yanayodaiwa na wakala huyo yatakapolipwa, na kwamba hatua ya MSD ni kuleta msukumo kwa taasisi za tiba kulipa madeni yao, na kuendelea kupata huduma kutoka MSD. " Kile kinachotokea kina madhara makubwa kama hakitashughulikiwa kwa uangalifu.Serikali inatakiwa kutoa fedha kwa wakati kwenda hospitali za umma ili ziweze kuilipa MSD."
Hivi karibuni MSD ilisema miongoni mwa taasisi za tiba zinazodaiwa na wakala huyo ni pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili kiasi cha shilingi bilioni 8 hali ambayo imesababisha MSD kusita kuendelea kununua dawa muhimu kwa ajili ya hopsitali hiyo zikiwemo dawa za kutibu wagonjwa wa figo.
Post a Comment