0

Kijana mmoja jana akamatwa katika msikiti wa Shafia uliopo Gongo la Mboto na kufikishwa kituo cha polisi cha Gongo la Mboto jijini Dar es salaam kwa tuhutuma za kutapeli msikitini ajifanya yeye ni Bubu akiomba asaidiwe msaada baada ya waislamu kumchangia lakini kijana mmoja alikuwa na wasiwasi nae kama anayeomba asaidiwe si bubu? kwani kijana aliyekuwa na wasiwasi nae aliwahi kusikia  kituo cha Radio Imaan kulipoti kuna mtu anatumia njia kama hii ya ububu kwa kutapeli ndipo alipobanwa akawa amejieleza kama yeye si bubu.Katika mahojiano na kijana huyo alikili kama yeye si Bubu na kazi hiyo ya utapeli ameweza kutapeli ndani ya miaka 2 toka mwaka 2012 na amewahi kutapeli maeneo mbalilmbali ikiwemo Lindi,Mbagala,Ubungo,Tanga,Morogoro na Nachingwea.
                           CHANZO:RADIO IMAAN

Post a Comment

 
Top