Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapa nchini Jaji Mstaafu Damian Lubuva
(katikati) akizungumza na waandishi wa habari jana, kulia ni Katibu
Tawala wa Mkoa wa Singida, Liana Hassan na kushoto ni Mkurugenzi wa
Manispaa ya Singida Joseph Mchina.
Na Hillary Shoo, SINGIDA.
TUME ya
Taifa ya Uchaguzi imeanza mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu
la wapiga kura,kwa kuwashirikisha kwa karibu waandishi wa habari hapa
nchini.
Lengo
la kuwashirikisha waandishi wa habari ni kutokana na uwezo na hekima
katika kupeleka taarifa na kuhamasisha jamii na wananchi kwa ujumla
kupitia vyombo vya habari.
Hayo
yamebainisha jana mjini hapa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati akifungua mkutano na
waandishi wa habari wa Mkoa wa Singida.
Jaji
Lubuva alisema lengo ni kuhakikisha kuwa wale wote wenye sifa za kuwa
wapiga kura wanajitokeza kwa wingi katika vituo vya kujiandikisha kwenye
daftari la kudumu la wapiga kura.
Aidha
alisema kuwa Tume inatarajia kufanaya uboreshaji wa Daftari la Kudumu
wa Wapiga kura kwa awamu ya kwanza hivi karibuni kwa kutumia Teknolojia
mpya ya Biometric Vote Regstration ( BVR).
Alisema
mfumo huo mpya ni wa kuchukua au kupima taarifa za mtu za kibaiolojia
au tabia ya mwanadamu na kuhifadhi katika kanzi data kwa ajili ya
utambuzi.
“Mfumo
huu hutumika katika kumtambua mtu na kumtofautisha na mwingine, ingawa
tabia hizo za binadamu ziko nyingi, lakini kwa ajili ya kuandikisha
wapiga kura alama za vidole kumi vya mikono, picha na saini ndizo
zitachukuliwa na kuhifadhiwa kwenye Kanzi Data (Database) ya wapiga
kura.” Alisisitiza Jaji Lubuva.
Hata
hivyo alisema kwa kutumia mfumo huu wa (BVR), wananchi wote wenye sifa
za kuwa wapiga kura na wale walio na kadi za mpiga kura watatakiwa
kuandikishwa upya.
Jaji
Lubuva alisema mafunzo kwa Watendaji yanatarajiwa kufanyika muda
kuanzia Mwezi Julai mwaka hauu kabla ya zoezi la uboreshaji wa Daftari
kufanyiaka.
Mwenyekiti
huyo alibainisha kwamba uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura
umeshafanyika na kwa sasa uandikishaji utafanyika katika vituo vilivyo
katika ngazi ya vitongoji, Vijiji na Mitaa.
“
Kutokana na utaratibu huu wa sasa vituo vya kujiandikisha vimeongezeka
kutoka 24,919 hadi kufikia vituo 40,015 ambavyo vimewekwa katika ngazi
za Vitongoji, Vijiji na Mitaa’. Alisema na kuongeza
“Ili
kuwezesha kuwa karibu zaidi na wanancahi na hivyo kupunguza malalamiko
ya auambali wa vituo vya kujiandikisha na kuaongeza mwamko wa
kujiandikishwa na kupiga kura.” Alifafanua Jaji Lubuva.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Joseph Mchina, alisema
maandalizi yote muhimu kwa ajili ya zoezi hilo katika Manispaa yake
yamekamilika na hivyo kuwa na vituo 154 badala ya 84 vya awali.
Post a Comment