Jamaa
wawili wanaotuhumiwa kuwa wezi, nusura wauawe kwa kuchomwa moto na raia
waliamua kuchukua sheria mkononi baada ya kula kichapo ‘hevi’ kwa msala
wa kukwapua mkoba wa mrembo aliyekuwa ndani ya Bajaj.
Kijana
ambaye hakufahamika jina lake mapema amejikuta kwenye mikono ya
wananchi wenye hasira kali baada ya kukwapua mkoba kwenye bajaji
Katika
tukio hilo lililojiri maeneo ya Kijitonyama, Dar, mwanzoni mwa wiki
hii, shuhuda aliyeona alisema aliwaona vijana hao wakiwa wamepanda
pikipiki wakipora mkoba wa mrembi huyo aliyejitambulisha kwa jina la
Magdalena John (21)
Alisema baada ya kupora mkoba huo walianza kutoka nduki lakini kabla hawajafika mbali, mtu mmoja aliyekuwa na gari, ambaye pia aliona tukio hilo, aliziba njia na kuwafanya vijana hao kutumbukia mtaroni.
msichana
huyo alishuka ndani ya Bajaj na kuanza kuwapigia kelele za wizi hivyo
kuwafanya wapita njia kuanza kuwapiga kwa kutumia silaha mbalimbali
zikiwemo mawe, fimbo na matofali.
Waandishi wa habari hii waliowahi kufika eneo la tukio, waliwashuhudia watu hao wakipokea kipigo kikali kilichowafanya wawe hoi.
Akizungumzia
mazingira ya tukio hilo, Magdalena alisema ana hofu kuwa waliompora,
walianza kufuatilia nyendo zake tangu alikotoka nyumbani kwake maeneo ya
Mwananyamala, Dar.
“Mimi naweza kusema huu ni mchezo ambao umepangwa tangu naanza safari, kwani wangejuaje kama nimeshikilia mkoba wakati nilikuwa ndani ya Bajaj?” Alihoji msichana huyo ambaye aliomba vijana hao wauawe.
Hata
hivyo, wakati jamaa hao wakipokea kipigo kutoka kwa wananchi, baadhi ya
watu walipiga simu Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar
ambao baada ya muda mfupi waliwasili wakiwa tayari kwa lolote.
Baada
ya kufika eneo la tukio na kuona namna vijana hao walivyokuwa
wamechakazwa, waliwachukua vijana hao na binti aliyeporwa kisha kuelekea
kituoni kwa mahojiano zaidi.
Lakini katika hali ya kusikitisha zaidi, baada ya vijana hao kupora mkoba huo na kutumbukia mtaroni, baadhi ya watu waliokuwa wakiwapiga, nao waliuchukua mkoba huo na kutoweka nao kusikojulikana.
Credits:GPL
Post a Comment