0

 Askofu Gervas Nyaisonga wa jimbo la Katoliki la Mpanda akisalimiana na Mapadri wa jimbo hilo katika eneo la mto koga Hapo jana ambapo ndipo linapoanzia Jimbo katoliki la Mpanda wakati alipokuwa akiwasili rasmi kwenye jimbo lake jipya la Mpanda akiwa anatokea jimbo la Dodoma 
 Askari  wa skauti wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda wakiwa katika eneo la daraja la mto koga wakimpokea askofu Gervas Nyaisonga alipowasili hapo jana akitokea jimbo la Dodoma ambapo askofu Nyaisonga alipokuwa analiongoza kabla ya kuhamishiwa Jimbo la Mpanda na amesimikwa jana kuwa askofu wa Jimbo la Mpanda

 Askofu Gervas Nyaisonga wa Jimbo katoliki la Mpanda akibusu Ardhi hapo jana katika kijiji cha Kamsisi ikiwa ni ishara ya kuhamia rasmi kuliongoza jimbo la Mpanda akitokea jimbo katoliki la Dodoma


 Msafara wa waendesha pikipiki wakiwa katika eneo la uwanja wa ndege mjini Mpanda wakiwa wanaongoza msafara wa kumpokea askofu Gervas Nyaisonga hapo jana ambae amehamishiwa jimbo la Mpanda akitokea jimbo la dodoma
 Mapadri wa kanisa katoliki wakiwa kwenye kanisa kuu la jimbo Katoliki la Mpanda kabla ya kuanza kwa ibada ya kukabidhiwa ufunguo wa kanisa hilo askofu Gervas Nyaisonga ambae amehamishiwa jimbo la Mpanda ikiwa ni ishara ya kuyaongoza makanisa na kuyasimamia makanisa yote ya jimbo katoliki la Mpanda 

Picha na Walter Nguluchuma 
Katavi yetu Blog
******************
Na  Walter Mguluchuma

Padri  wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Mpanda Padri Matini Kapufi (42 ) pamoja na Katekista wa Kanisa hilo  wa KijiJI  cha  mtakuja  Parokia ya Inyonga  Katekista Patricki Mwendo  wa Saa (60) wamefariki   Dunia  baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka  baada ya gari kuacha  njia na watu wengine wawili kujeruhiw na kulazwa hospitalini

Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri  Kidavashari ajari hiyo ilitokea hapo juzi  majira ya saa  nne asubuhi  katika Kijiji  cha Kamsisi   tarafa ya Inyonga barabara  ya  Inyonga  kuelekea Mkoani Tabora

Alisema ajari  hiyo ililihusisha gari aina ya  Toyota  Hilux pick Up  lenye  namba za usajiri  T 302 CUY lililokuwa likiendeshwa na  Marehemu Padri Martini Kapufi  ambae ni Paroko wa parokia ya Mwese  jimbo katoliki la Mpanda


Kidavashari  aliwataja watu   waliojeruhiwa kwenye ajari hiyo kuwa ni Daud Saveli  (31)  katekista msaidizi wa kijiji  cha Mtakuja parokia ya Inyonga, ambae ameumia sehemu ya kidevu chake na mguu wa kushoto  na melikio  Maraluma  mkazi wa kiji cha mtakuja Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele

Alisema  watu hao walipata ajari  wakati  wakiwa wanasafiri kutoka Inyonga  makao makuu ya Wilaya ya mlele  wakiwa wanaelekea eneo la Mto Koga mpakani  mwa Mkoa wa Katavi  na Tabora kwa lengo  la kwenda kumpokea Askofo Gervas Nyaisonga  aliyekuwa  akitokea Dodoma ambae ameamishiwa jimbo la Mpanda akitokea jimbo katoliki la Dodoma

Kamanda Kidavashari  alieleza  kuwa  watu hao  ndipo walipokuwa wakisafiri   na gari hiyo  na walipofika katika maeneo ya kijiji cha Kamsisi  gari hiyo iliacha njia na kupinduka ambapo  Katikista Patrick  Mwendowasaa alifariki hapo  hapo mara baada ya kutokea kwa ajari na Padri  Martini Kapufi alifariki njiani wakati akiwa anapelekwa kwenye kituo cha afya  cha Inyonga

Alisema majeruhi  wote wawili wamelazwa katika  kituo cha afya  cha Inyonga  wakiwa wanaendelea kupatiwa matibu huku  hali zao zikiwa zinaendelea vizuri na miili ya marehamu hao wawili imehifadhiwa katika  chumba cha kuhifadhia maiti cha kituo cha afya cha Inyonga

Kamanda Kidavashari alieleza     kitengo cha jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani  kinaendelea na uchunguzi  ili  kuweza kubaini chanzo kilichosababisha ajari hiyo ya gari mali ya jimbo Katoloki la  Mpanda.

Post a Comment

 
Top