Jaji wa mahakama nchini Misri, amewahukumu kifo watu 683 akiwemo kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood Mohammed Badie.
Mawakili
wa watuhumiwa wanasema kuwa wateja wao walikabiliwa na makosa mengi
yakiwemo, kushambulia kituo cha polisi mjini Minya mwaka 2013 ambapo
polisi mmoja aliuawa.
Kesi na
kasi ya kuzisikilizwa kwa kasi hizo, imesababisha hasira na kukosolewa
na shirika la kutetea haki za binadamu la Umoja wa Matifa UN.Jaji huyo
pia alibatilisha hukumu ya kifo iliyotolewa kwa watu 492 kati ya watu
529. Hukumu hiyo ilipitishwa mwezi Machi na sasa watahudumia kifungo cha
maisha jela.
Post a Comment