RAIS Jakaya Kikwete, ametoa msamaha kwa wafungwa 3,967 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana
na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, Rais ametoa
msamaha kwa wafungwa kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya ibara ya 45
(1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia Rais Kikwete amepunguzia wafungwa wote moja ya sita ya vifungo
vyao zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa chini ya kifungu 49 (1)
cha Sheria ya Magereza sura ya 58 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa
katika Ibara ya 2(1-xviii).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo wafungwa watakaopata msamaha huo ni wale
wenye magonjwa ya Ukimwi, kifua kikuu na kansa, wazee kuanzia umri wa
miaka 70 na zaidi ambao wamethibitishwa na jopo la waganga chini ya
uenyekiti wa mganga mkuu wa mkoa au wilaya.
Post a Comment