Wanajeshi wa Kenya waliopo AMISOM
Wafanyakazi
raia wa Kenya wa mashirika ya misaada ya kibinadamu ambao walikuwa
wametekwa na wapinaji wa kiislamu wa Al shabaab mwaka 2011 wameokolewa
na majeshi ya Kenya.
Daniel
Njuguna ambaye alikuwa akifanya kazi katika shirika la Madaktari wasio
na mipaka Medecins Sans Frontieres MSF na James Kiarie wa Shirika la
Care International, walichunguzwa afya zao na walitarajiwa kusafirishwa
kwenda Nairobi.
Awali walikuwa chini ya uangalizi wa
majeshi ya Kenya ambalo lipo kwenye kikosi cha Umoja wa Afrika kilichopo
nchini Somalia AMISOM.Kenya ilituma majeshi yake kwenda nchini Somalia mwaka 2011 kujiunga na AMISOM kufuatia matukio ya utekaji nyara yaliyokuwa yakiendeshwa na wapiganaji wa Al shabaab katika mipaka ya nchi hiyo na Somalia.
Majeshi ya AMISOM yakishirikiana majeshi yale ya serikali ya Somalia yamekuwa yakiendesha mapambano dhidi ya wapiganaji wa Al Shabaab ambao wanafadhiliwa na kundi la kigaidi la al Qaeda linaloshikilia maeneo ya kusini na katikati mwa Somalia.dj sek
Post a Comment