Jana
April 16 2014 UKAWA wakiongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba wakati bunge
likiwa katikati waligoma kuendelea nalo na kuamua kutoka nje kwa kile
wanachosema ni ubaguzi na matusi pamoja na mapungufu mengine ambayo
hawawezi kuyavumilia.
Baada
ya hayo mwenyekiti wa bunge la katiba Mh. Samwel Sitta leo April 17
2014 akatumia sekunde kadhaa tu baada ya bunge kuanza kwa kusema ‘jana
kumetokea jambo moja la kusikitisha na kwa hakika baadhi yetu
tumesononeka sana na tukio la jana la wenzetu wanaitwa UKAWA kutoka nje
ya ukumbu huu na hadi sasa hawajaniambia kama wametoka moja kwa moja au
vp, kwa vyovyote vile jambo lile halikustahili’
‘Katika
nchi yoyote kwa Mwananchi kuteuliwa kuwa miongoni mwa wale ambao
wanaaminiwa na nchi kutunga katiba mpya ya nchi ni heshima ya kipekee
kabisa, ni dhamana ambayo inatakiwa kuchukuliwa kwa uzito wowote kwa
sababu utungaji wa katiba ni jambo la mara moja pengine kwa vizazi
viwili vitatu’
‘Nilivyokua
naangalia jana katika TBC1 maelezo yaliyotolewa na kiongozi wa UKAWA
Prof. Ibrahim Lipumba kwamba wametoka kwa sababu ya lugha ya matusi na
ubaguzi, kwa sababu ya Waziri mmoja wa serikali yetu amenukuliwa katika
gazeti eti kasema mambo ambayo wao yamewaudhi yanadhihirisha ubaguzi
bila hata Waziri huyo kupewa nafasi ya kueleza aliyoyasema’
‘Tumemuita
Mh. Lukuvi alikua anaelekea Airport kwa matibabu, tumemuita arudi hapa
na atatoa maelezo ambayo kama ni yale aliyoniambia mimi basi sijui watu
walimnukuu vipi mpaka wenzetu kuona kwamba aliyoyasema yamewaudhi kiasi
hicho lakini ukweli utabainika’
‘Wakati
wote tumeushuhudia mwendelezo ambao tumeendelea kuuvumilia kwa nia
njema kwamba tufikie mwisho mwema wa kutunga katiba, nyinyi nyote
mnafahamu kanuni za bunge hili maalum zinapendelea wachache na tumefanya
hivyo makusudi, ofisi yangu imekua wazi kupokea malalamiko ya yeyote
ambae kaonewa’
‘Nimeitisha
mkutano wa dharura wa kamati ya uongozi ili tuweze kuelewana namna ya
kushughulikia jambo hili, ikiwa wenzetu wanatusikia na ikiwa bado wako
Dodoma kwa sababu baadhi yao ni wajumbe wa kamati ya uongozi, waje
watueleze kwa undani hatma ya vitendo vyao kwa sababu vina athari
kisheria na kiutawala, wamejiuzulu au kutoka nje kuonyesha hisia zao
alafu watarejea?’ wawepo ili tuzungumze tusaidiane’
‘Kazi
iliyopo mbele yetu sio kazi ambayo unaweza kuisusa tu, mi sipendi
niingie katika kauli matusi na ubaguzi lakini katika maeneo ya haki za
binadamu, mtu anaedai kabaguliwa alafu anaondoka na kundi lake wanaimba
Interahamwe, huu ni mwaka wa 20 toka mauaji ya Kimbari kule Rwanda, na
neno iterahamwe hapa Afrika ni tusi la mwisho kabisa kwa sababu lina
maana ya mtu mwenye chuki ambae yuko tayari kutekeleza mauaji tena ya
Kimbari’
‘Sisi
tumevumilia hata jina la mkusanyiko wao, (UKAWA) wao wanadai ndio umoja
wa katiba ya Wananchi kama vile tunachokifanya humu sio cha Wananchi
lakini tumevumilia tu manake hata jina hilo ni la kibaguzi, itakuaje
kikundi kitoke nje chenyewe ndio kiseme ndio kinatunga au kinasimamia
Wananchi kuliko sisi wengine wote tuliomo humu’
‘Sababu
za kitendo chao jana hazitoshi, mlango wangu uko wazi na nimeongea pia
na Waziri mkuu, yeye kama kiongozi pia wa chama cha mapinduzi pia mlango
wake uko wazi, kama kuna jambo limejificha tujadiliane ili turudi
kuendelea kutunga katiba ya Wananchi’.vijana na matukio
Post a Comment