Meli ya Korea Kusini ikizama.
Watu
walionusurika wamekuwa wakielezea hali ilivyokuwa ya kutisha ndani ya
meli ya Korea Kusini ilipoanza kusimama kwa kuyumba, akiegemea upande
mmoja na haraka kuanza kuzama."Kwa kweli kulikuwa na sauti kubwa na meli ghafla ikanza kuegemea upande mmoja," amesema abiria aliyeokolewa, Kim Song-Muk.
"watu walikuwa wakihangaika kukimbilia maeneo ya juu ya meli, lakini ilikuwa vigumu kufanya hivyo kutokana na meli kupinduka."
Bado
haijafahamika kilichosababisha kuzama kwa meli hiyo, ambayo kwa kiasi
kikubwa iliwabeba wanafunzi wa shule, lakini watu walionusurika katika
ajali hiyo wanatoa maelezo sawa kuhusu tukio hilo la kutisha.
Kikosi
cha Walinzi wa Pwani ya Korea Kusini kimesema abiria wapatao mia tatu
hawajulikani walipo baada ya meli kupinduka na kuzama.
Watu
wawili wamefahamika kupoteza maisha na watu mia moja na sitini na wanne
wameokolewa. Kikosi cha wapiga mbizi kwa sasa wanatafuta meli iliyozama.
Wengi wa abiria wa meli hiyo ni wanafunzi wa sekondari wakiwa katika
safari ya masomo kuelekea kisiwa cha Jeju, nchini Korea Kusini.
Meli hiyo ilikuwa na watu 460.
CHANZO NI BBC SWAHILI
Post a Comment