Ilikuwa
Mida ya Saa tatu za asubuhi ambapo Magari zaidi ya 10 ya Jiji yalikuwa
yamejipanga eneo la mwenge Huku kukiwa na Ma Askari wa FFU wa kutosha
pamoja na Migambo wa Jiji huku wakiongozwa na watu wa Jiji kwa ajili ya
Kukamilisha swala zima la bomoa bomoa vibanda vyote ambavyo havina
mpangilio.
Mgambo
wakiondoa mikokoteni na kuipakia kwenye gari bada ya kufanya zoezi zima
la bomoabomoa eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo lilianza
kwa utulivu na kuendelea kwa utulivu kutokana na ulinzi mkubwa
uliokuwepo huku wananchi wakiendelea na kazi zao kama kawaida na
kukatazwa kukatiza katika eneo la tukio kwa usalama wao
Hata
hivyo Baada ya vibanda hivyo kutolewa kumegundulika kuwa kulikuwa ni
kuchafu kupindukia kutokana na uchafu uliokuwa umezagaa kila kona.
Kulia ni Magari mbalimbali ya Serikali yakiwa yamepaki eneo la Mwenge huklu zoezi likiendelea
Akina
Mama eneo la Mwenge wakihangaika kutoa vitu vyao baada ya Bomoa Bomoa
kupita..Hawa ni wale wauza Chai na Supu asubuhi na hata chakula cha
mchana
Huwezi
amini lakini ndio hali halisi sasa eneo jirani na Kituo cha Mabasi
Mwenge hakuna tena Adha ya vibanda , lakini umebaki uchafu uliopitiliza
na kugundulika kuwa hawa watu walikuwa wakifanya Biashara katika maeneo
ambayo si salama
Hili ni
eneo ambalo lilikuwa ni maarufu kwa ajili ya kuuza vitu mbalimbali kama
nguo na viatu vya mitumba lakini kwa sasa hakuna kitu ni peupe
Kwa wale
akina dada hili lilikuwa eneo maarufu sana kwa ajili ya Kutengenezea
nywele na saloon bubu ambazo zote zimevunjwa vunjwa kwa sasa
Hapa juu
mwanzo kulikuwa na mabanzi ya kutosha na wakina dada wengi walikuwa
wanapenda kuwa hapa wakitengenezwa nywele zao wasijue kuwa walikuwa
wakikaa katika eneo chafu kama hili.
Gari hili likijiandaa kuondoka baada ya somba somba
Kwa
kuliangalia Eneo hili utasema ni chafu sana lakini ndio ambalo lilikuwa
maarufu hasa kwa akina mama na akina dada kutengenezea kucha zao na
kusuguliwa miguu, Je kama wangejua ni pachafu hivi wangeweza kugusa hata
kuja kutengeneza kucha?
Bomoa bomoa ikiendelea
Baada ya
kufanya manunuzi watu hutupa takataka tuu, zilikuwa zikijificha
kulingana na mkusanyiko wa watu lakini hii ndio hali halisi sasa
Hakuna Vibanda lakini adha imebakia sasa ni ya uchafu
Je hapa tutapona magonjwa ya mlipuko?
Sehemu hii ya stendi ya Mwenge ni peupe kuna nafasi ya watembea kwa miguu
Huu ni
upande wa pili wa kuelekea Mikochemi ambapo bajaji Hupaki napo
wamesafisha kwa kubomoa vibanda vyote hapa ni Shwari peupe
Picha
hizi mbili ni eneo maarufu sana ambapo watu walikuwa wanauza Vifaa vya
umeme na DVD, Sub Woofer pamoja na Radio bila kusahau TV sasa pamebaki
kama hivi, Je walikuwa hawajui kama ni pachafu kiasi hiki?
Picha na Pamoja Blog/ Dar es salaam yetu Blog
Post a Comment