Mhe.
Mufti Sheikh Issa Shaaban Simba akimkaribisha Mwenyekiti wa Bunge
Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta leo jijini Dar es Salaam wakati
alipomtembelea kumuelezea maendeleo ya vikao vya Bunge linaloendelea
mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta (kulia) akiongea na
waandishi wa habari mara baada ya ziara yake katika Ofisi za Bakwata
kuelezea maendeleo ya Kikao vya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma.
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Bakwata Suleiman Lolila.(PICHA ZOTE NA BUNGE
MAALUM LA KATIBA).
Na. Benedict Liwenga-Maelezo
MWENYEKITI
wa Bunge maalum la Katiba Samweli Sitta amesema katiba mpya ni kwa
manufaa ya wanachi wote kwa ajili ya kuwaletea maendeleo katika nyanja
mbalimbali.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam alipokutana na Mhe. Mufti Sheikh
Issa Shaaban Simba katika Ofisi za Bakwata zilizoko Kinondoni jijini
Dar es Salaam ikiwa ni utaratibu aliojiwekea kwa ajili ya kuwashirikisha
Viongozi wa madhehebu na dini ili nao wapate taarifa ya maendeleo ya
bunge la katiba.
Mhe.
Sita amesema kuwa Viongozi wa dini ni watu muhimu sana kwakuwa wanabeba
wafuasi wengi katika jamii na kuwepo kwao kunasaidia katika maendeleo
ya nchi hususani kujenge Amani ya nchi yetu na kuwahamasisha wananchi
kuwa wavumilivu, watulivu, waelewa na wenye kupenda Amani.
Namuomba
Mhe. Mufti pamoja viongozi wengine wa dini waizidi kutuombea ili tuweze
kufikia muafaka katika kupata katiba mpya na bora yenye kuleta
mabadiliko katika nch yetu” Alisema Mhe. Sitta.
Mhe.
Sita Ameongeza kuwa Watanzania wanataka katiba itakayoijenga Taasisi
imara zitakazoweza kusimamia mambo muhimu na kuweza kuondokana na
uhalifu ikiwemo janga la madawa ya kulevya ambalo limekuwa likiisumbua
sana nchii kwa msaada wa sheria mpya janga hili linawezekana
kudhibitiwa.
Pia
amewaomba wajumbe wa kamati kumi na mbili za bunge la katiba,wasome kwa
makiini ibala ya sura ya 1 na ya 6 ambazo ni muhimu sana katika
kuijenga nchi, ili waweze kutoka na mawazo mazuri na yakinifu kwa
manufaa ya nchi na watu wake na kuweza kukuza uchumi na kuleta
maendeleo.
“Katiba
itunge sheria ambazo ni imara zenye kufuata kanuni na taratibu dhabiti
ili kuleta mabadiliko katika kuiongoza nchi na kuweza kuwasaidia
wananchi wake” Alisema Mhe. Sitta.
Aidha,
ameongeza kuwa Bunge hilo maalum linatarajia kuhailishwa mwezi wa nne
tarehe 28 kwa ajili ya kupisha bunge la Bajeti,na kwa kuwa siku 70
hazitoshi kumaliza bunge hilo amemuomba Mheshimiwa Rais Kuwaongezea muda
hivyo wanatarajia kurudi tena mwezi wa nane kuweza kuendelea na
mijadala ya katiba mpya.
Post a Comment