Mwenyekiti
wa Wabunge Wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna
Abdallah ametoa wito kwa wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba
kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuhakikisha kuwa wanaweka maslahi ya
mwanamke mbele katika uandishi wa Katiba mpya na sio vinginevyo.
Mwenyekiti
huyo ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati anafungua semina ya siku
moja ya wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba iliyoandaliwa na
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini (TAMWA) kwa lengo la
kuwaelimisha juu ya kuwepo na haja ya kuwepo na vipengele vinavyotetea
haki za wanawake na watoto katika masuala mbalimbali.
Alisema
kuwa wajumbe hao wanawanawake wanapaswa kuweka kando tofauti zao za
kivyama, kiitikadi na kiimani na kuhakikisha kuwa haki za msingi
zinaweka katika Katiba mpya itakayotunga ili kujenga usawa wa kijinisia
katika masuala mbalimbali hapa nchini.
Anna
Abdallah aliongeza kuwa ni vema wajumbe hao wakatumia fursa hiyo
wliyoipata ya kuingia katika Bunge hilo maalum katika kuhakikisha kuwa
vipengelea vinavyolinda haki za Wanawake na watoto na kupigania uwepo wa
usawa wa asilimia hamisni kwa hamisi katika masuala mbalimbali.
Aidha
aliongeza kuwa ni jukumu la wanawake wote walioko katika madaraka
kuwatetea wanawake wengine ambao wako nje na hata kuwahamasisha kwa
kuwapa moyo wa kuingia katika siasa na kuwania madaraka mbalimbali
badala ya kuwakatisha tama.
Akitoa
mada katika Semina hiyo Mkurugenzi Mttendaji wa TAMWA Valerie Msoka
alisema kuwa ni vema wajumbe hao wakapigani wazi umri wa mtoto uwekwe
wazi na pia umri wa kuweza kuoa na kuolewa.
Aliongeza
kuwa mambo mengine ni pamoja na kuweka vipengele vinavyopinga ukatiili
wa kijinsia kama vile kupinga ndoa za utotoni, ukeketaji , kulazimishwa
biasha ya mapenzi na ubakaji.
Naye
Makamu Chansela wa Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki Profesa Esther Daniel
alisema kuwa suala la uzazi salama ni muhimu likazingatiwa katika
uandishi wa Katiba mpya ili kuzuia mimba za utotoni na vifo
vinavyotokana na uzazi.
Post a Comment