Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani unaanza wiki hii duniani kote, watu wenye imani ya dini ya kiislamu watajizuia kula chakula na kunywa tangu kuchomoza mpaka kuzama kwa jua.
Malengo haya ni katika kutimiza nguzo za uislamu kwa kuswali na kujizuia ,wakati kipindi hiki kikitazamwa kama nafasi ya kujisafisha kiroho.
Wakati kwa mtazamo wa kawaida linaonekana kama jambo rahisi, kuna imani chache na upotoshaji uliosabisha uwepo wa maoni tofauti kwa miaka mingi.
Yafuatayo ni mambo sita kati yao,sambamba na uchambuzi wa Shabbir Hassan, Mwanafunzi wa sayansi ya dini ya kiislamu na sharia, na Hafidh wa Koran, maana yake amehifadhi Korani yote
Miswaki
Kusafisha meno hakubatilishi funga yako, kwa mujibu wa wasomi.
Hassan anasema mara chache watu hufunga wakiamini kuwa ladha ya dawa ya meno inatosha kubatilisha funga
Ingawa wasomi wengi wa maswala ya dini watakubalina kuwa kusafisha meno yako ni sawa, Bwana Hassan ana vidokezo kadhaa kwa wale walio na wasiwasi.
''Ushauri mzuri ni kutumia dawa ya meno kwa kiasi kidogo, tumia kitu ambacho hakina harufu kali.
Pia ameshauri kutumia miswaki ya miti yenye ladha ya asili, miti hii pia inaelezwa na shirika la afya duniani kuwa ni salama kwa matumizi ya mdomoni.
Kumeza mate yako mwenyewe inaruhusiwa na pia inashauriwa kufanya hivyo
''madai haya hayana msingi kabisa, ameeleza Bwana Hassan, ''kumeza mate yako ni suala la asili halizuiliki hivyo halibatilishi funga.
Kitakachobatilisha funga ni kumeza mate ya mtu mwingine jambo ambalo linapaswa kuzuiwa
Hautaruhusiwa kumbusu mweza wako au mke wako,Mantiki nzima ya kufunga ni kudhibiti hisia, vikiwemo chakula, vinywaji na kuwa na wapenzi.
Kula au kunywa si maswala pekee ambayo yataharibu funga
Maswala mengine yanahusisha ''Dhambi inayotekelezwa na ulimi'', alieleza Bwana Hassan, dhambi hiyo ni kama vile kusengenya, kujiapiza kwa watu wengine na kufitini.
Kama kweli ulisahau kabisa kuwa ulikuwa umefunga kisha ukala kitu, funga yako bado itahesabiwa kuwa halali, ilimradi tu uliacha mara moja baada ya kugundua.
Hata hivyo, kama kwa bahati mbaya umekula kitu katika mazingira ambayo yangeweza kuzuilika, kwa mfano wakati wa kutawadha kabla ya swala, basi funga yako ni batili.
moja kati hatua nane za kutawadha ni pamoja na kusukutua kinywa, kisha kwa bahati mbaya ukameza maji kutabatilisha funga yako.
Bwana Hassan anaeleza wakati wa kutawadha wakati umefunga, unatakiwa uepuke kusukutua, unashauriwa kuweka maji mdomoni na kutema mara moja.
Baraza la Kiislamu nchini Uingereza (MCB) lilitoa angalizo sambamba na shirika la kimataifa la afya ya macho wakiwataka watu kuendelea kutumia dawa kama vile za matone.
MCB pia imetoa mwongozo mwezi wa ramadhani kwa ajili ya matumizi ya hospitalini, ikieleza kuwa matone ya macho, sindano ni miongoni mwa tiba zisizoharibu funga.
Hata hivyo, kumeza dawa kutaharibu funga, inashauriwa kumeza dawa kabla na baada ya kufunga
Hassan anasema ''kwanza, kama una tatizo la kiafya,swali la kuuliza ni je ninaweza kufunga?
Koran inasema wazi kuwa usikilize ushauri wa Daktari''.
Katika uislanu, kufunga ni wajibu kwa wale walio na afya njema na wamefikia umri wa utu uzima, kwa kawaida miaka takribani 15.
Hii haiwahusishi watoto na watu walio wagonjwa, (kimwili na kiakili), wanaosafiri, waja wazito na wanaonyonyesha, kwa mujibu MCB.
Kuna njia nyingine watu wazima wanaoshindwa kufunga wanaweza kupata thawabu wakifanya, bila kujiweka hatarini
''Kama ni ugonjwa wa muda mfupi wanajua watapona basi watafunga siku nyingine, alieleza Bwana Hassan
Kama ni maradhi ya muda mrefu anaweza kutoa Fidia, mchango mdogo unaotolewa kwa siku, ambapo utakuwa ukilisha familia masikini
Post a Comment