0



Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii, MOSHI

CHUO cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Moshi kimeaanzisha na kuendeleza mafunzo ya kozi ya Uzalishaji mvuke yenye fursa kubwa katika soko pamoja na kozi ya mitambo katika uchimbaji wa madini ambao umetoa ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi habari waliotembelea katika Chuo cha VETA Moshi, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Douglas Mlulla amesema moja ya mafanikio yao ni kwamba vijana wanaosoma hapo wana uhakika wa ajira za moja kwa moja kutokana na ushirikiano na kampuni za uchimbaji madini.

Amesema VETA Moshi ni chuo kina kozi ambazo zina wigo mkubwa wa ajira katika uchimbaji wa madini, pamoja kozi uzalishaji mvuke ambapo sehehu ya viwanda vya vinywaji ni lazima kuwepo kwa wataalam wa kozi hiyo.

Hata hivyo amesema mwitikio wa vijana ni mdogo kutokana na kutofahamu umuhimu wa ufundi stadi ambao ndio unaajiri watu kwa sehemu kubwa, hivyo ameashauri vijana kuchangamkia fursa hata kama anashahada ni vema akaongeza na mafunzo ya ufundi stadi.

Pia amesemakozi ya Uendeshaji wa mitambomikubwa imeonekana kuvutia vijana wengi wakiwemo wasichana.Mmoja wanafunzi wa kozi hiyo, Happiness Steven amesema yeye anashahada ya kwanza rasilimali watu na baada ya kuona changamoto ya ajira ameamua kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi na kufanikiwa kupata kazi katika kiwanda na kuwa afisa uajiri katika kiwanda hicho.

Amesema kozi ya uchomeleaji na uchongaji wa vyuma alivutiwa na kuamua kujiunga nayo licha ya mtazamo uliokuwepo kwa muda mrefu kuwa hiyo ni kozi kwa ajili ya wanaume.Amesema waliohitimu Shahada wajiongeze katika ufundi stadi na hatimaye changamoto ya ajira watakuwa wameimaliza kwani hakuna kazi isipokuwa ni watu kuchagua kazi za kufanya kwa taaluma waliozonazo.

Kwa upande wa Mratibu wa Mradi wa IMTT Chuo hicho,Theresia Mosha amesema ushirikiano kati yao na kampuni za uchimbaji madini umetoa fursa vijana wengi waliopita katika mradi huo pamoja na waliosomea kozi ya uzalishaji mvuke kupata ajira.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Moshi , Douglas Mlulla akizungumza na waandishi habari walipotembelea chuo hicho kuhusiana na fursa ambazo zinapatikana katika chuo.
.Afisa Rasilimali Watu wa Kiwanda cha Press , Forge & Metal Works (PFM2000) na Munufaika mafunzo ya ufundi Stadi VETA Moshi, Happiness Steven akizungumza wa kuhusiana na vijana kuchangamkia kozi ya ufundi stadi licha ya kuwa na shahada walizozipata.
Munufaika mafunzo ya ufundi Stadi VETA Moshi Happiness Steven akionesha  umahiri alioupata katika mafunzo ya ufundi Stadi katika chuo cha VETA Moshi.
Mwanafunzi wa kozi ya Mitambo Mikubwa,Happiness Rwechungura akioneha jinsi wanavypata mafunzo ufundi stadi katika chuo cha VETA Moshi.
Mkufunzi wa Kozi ya Mtambo wa kuzalishaji Mvuke , Mosana Marcus akionesha jinsi mtambo unavyoweza kuzalisha mvuke

Post a Comment

 
Top