Meneja wa Hoffenheim Julian Nagelsmann amepuuzia taarifa zinazomhusisha na uhamisho kuelekea timu za Arsenal and Chelsea. (Sky Germany via Daily Star)
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameunga mkono mlinzi raia wa Ujerumani anayekabiliwana shutuma Shkodran Mustafi, mwenye umri wa miaka 26, kusalia kwa muda mrefu huko Emirates. (Independent)
Gunners wamo katika hatari ya kumpoteza kipa wa England mwenye umri wa miaka 17 Arthur Okonkwo kwasababu bado anatarajiwa kutia saini mktana katika klabu hiyo. RB Leipzig na Celtic zote zinamuwania mchezaji huyo. (Mirror)
Meneja wa Everton Sam Allardyce amesema mzozo wake na meneja wa Newcastle Rafa Benitez wakati walipokuwa wakisimamaia klabu ya Bolton na Liverpool mtawalai ulitokana na kwamba "nilikuwa na mghadhabisha yoyote niliyeweza kumghadhabisha". (Shields Gazette)
Benitez, mwenye urmi wa miaka 58, anatafuta uungwaji mkono kutoka mmiliki wa klabu ya Newcastel - Mike Ashley kabla ye kuongeza muda wa kuhudumu katika klabu hiyo baadaya timu hiyo kushikilia hadhi yake katika Premier League kwa msimu mwingine. (Guardian)
Mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah amemtakia kheri mchezaji wa Arsenal wa kiungo cha kati Mohamed Elneny, mwenye umri wa miaka 25, aliyecheza naye huko Basel, baada ya kujeruhiwa alipocheza mechi dhidi ya West Ham Jumapili. (Metro)
Meneja wa Roma Eusebio di Francesco amesema hajawauliza wachezaji wake siri ya kumzuia Salah huku mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa ukitarajiwa. (Liverpool Echo)
Mchezaji mahiri wa Brazil Ronaldinho amedokeza kuwa mchezaji wa Manchester United Paul Pogba huenda akashinda tuzo ya Ballon d'Or - iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 atamsikiliza kwa makini meneja wake Jose Mourinho. (Canal Football Club via Goal)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester City Kevin de Bruyne, mwenye umri wa miaka 26, anasema ahisi 'tofauti' kama mshindi wa ligi ya England. (Manchester Evening News)
Spurs na Chelsea wanamwinda mchezaji wa Paris St-Germain mwenye umri wa miaka 25 Layvin Kurzawa - na Manchester United pia wanamtaka mchezaji huyo raia wa Ufaransa. (Mirror)
Mustakabali wa mlinzi wa Everton Luke Garbutt katika klabu hiyo unaonekana kumalizika baada ya mchezaji huyomweny eumri wa miaka 24 kuambiwa na Allardyce atafute klabu nyingine. (Liverpool Echo)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Sevilla Steven N'Zonzi, ameomba radhi kwa mashabiki wa klabu hiyo kwa kwenda kusherehekea Jumamosi usiku baada ya klabu hiyo kufungwa 5-0 na Barcelona katika fainali za taji la Copa del Rey. (Football Espana)
Meneja Mauricio Pochettino amekiri kuwa atafikiria kuwachezesha vijana wa Tottenhamkatika msimu ujao wa taji la FA. (Daily Mail)
Post a Comment