0
Tokeo la picha la barabara ya liwale

WAKALA wa barabara za vijijini na mijini (Tarura) mkoani Lindi,umetengewa Sh,7,451,487,000/-kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo,ikiwemo matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2017/18.
Mratibu wa mkoa huo,Agather Mtalyambate ameyaeleza hayo alipokuwa anatoa taarifa ya utekelezaji kikao cha pili cha Bodi ya barabara {Roadbod},kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Lindi.
Taarifa ya Mratibu huyo,iliyowasilishwa kwa niaba yakeo na,mwandisi Aloyce Nombo,imesema fedha hizo zitatumika kufanya matengenezo na usimamizi wa miradi ya barabara zilizopo vijijini na mijini ndani ya mkoa huo.
Nombo akiwasilisha taarifa yake hiyo,Nombo alisema kati ya kiasi fedha hizo,Sh,7,029,737,000/-kwa ajili ya matengenezo na usimamizi wa miradi ya barabara,wakati Tsh,422,750,000/-zimepangwa kufanya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha,aliwaambia wajumbe wa kikao hicho kuwa hadi kufikia mwezi februari mwaka huu,Tarura mkoa imeweza kupokea kutoka Serikali kuu kiasi cha Sh,3,993,106,500/-sawa na asilimia 54% ya bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18.
Mwandisi Nombo alitaja changamoto zinazoikabili Tarura mkoa ni pamoja na kukosekana vyumba vya kutosha kwa ajili ya Ofisi na baadhi ya wakurugenzi wa Halmashauri kutohamisha fedha za matazamio za wakandarasi {retention money} Sh,153,521,640/-kutoka akaunti za Amana na kuingiza za Tarura.
Halmashauri zilizotajwa kutotekeleza utaratibu wa kuzihamishia fedha hizo na viwango vyao ni,Kilwa Sh,81,183,379/-na Ruangwa {Sh,72, 338,270}.

Post a Comment

 
Top