Image captionNkurunzinza amekuwa rais wa Burundi tokea mwaka 2005
Chama tawala nchini Burundi CNDD/FDD kimemtangaza Rais Pierre Nkurunzinza kama kiongozi mkuu wa kudumu au kiongozi wa milele ndani ya chama hicho.
Uamzi huo umefikiwa baada ya vikao vya siku tatu vya mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika katika eneo la Buye anakozaliwa Bwana Nkurunziza Kaskazini mwa nchi hiyo.
Uamuzi huo pia unachukuliwa wakati Burundi inajiandaa kufanya marekebisho ya katiba ili kumruhusu Rais Nkurunzinza kuendelelea kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.
Taaarifa fupi ya chama cha CNDD/FDD imesema vikao hivyo vilinuwia kuimarisha chama tawala na taasisi zake.
Image captionAlinusurika kupinduliwa mwaka 2015
Lakini pia chama hicho tawala kimechukua uamuzi wa kumuongezea hadhi na kumpa cheo cha juu Rais Nkurunziza na hivyo kumtangaza kuwa ni kiongozi mkuu wa kudumu ndani ya chama.
Kwenye hafla na makundi ya utamaduni ya chama tawala, katibu mkuu wa CNDD/FDD Bwana Evariste Ndayishimiye aliutangazia umati azimio hilo alolitaka kuwa ni muhimu mno katika uhai wa chama tawala.
Tangazo hili la chama tawala CNDD/FDD kumfanya Rais Nkurunzinza kama Kiongozi Mkuu wa Kudumu linajiri wakati Burundi inajiandaa kwa kura ya maoni kuhusu Marekebisho ya Katiba baadae mwezi Mei. Kati ya mambo mengi katiba hiyo ikipitishwa itamuwezesha Rais Nkurunzinza kuweza kuwania Urais mpaka mwaka wa 2034.
Image captionNkurunzinza ni mcheza soka mashuhuri pia nchini Burundi
Wadadisi wengi wa siasa za Burundi wanaamini kuwa hatua hii ya chama tawala inanuwia kumalizia mapema mjadala wa mtetezi wa kiti cha Urais kwa niaba ya Chama hicho na kuonyesha mustakabali wa uongozi kabla hata uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2020.
Lakini pia uamzi huo unapeleka ujumbe kwa wafuasi wa CNDD/FDD na haswa viongozi wenye nia pengine ya kuwania nafasi hiyo na hivyo kujaribu kukiepusha chama tawala na mpasuko kama ilivyotokea mwaka wa 2015 katika mzozo kuhusu muhula wa sasa wa Rais Nkurunzinza.
Isitoshe kwa Wachanganuzi wa siasa za Bado wanaiona hatua hii ya Rais Nkurunziza kutangazwa Kiongozi wa maisha kama dalili tosha ya jinsi kiongozi huyo alivyokidhibiti chama cha CNDD/FDD.
Msanii mkongwe wa BongoFleva nchini Afande sele atangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) mwezi huu march mbele ya Rais Dkt. Maguf...Read more »
Mfanyabiashara maarufu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Moise Katumbi ambaye sasa amejitosa kwenye ulingo wa siasa, anazindua chama chake a...Read more »
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro baada ya Tume ya Uchaguzi (Nec), ...Read more »
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionTrump ana handaki ndani ya nyumba yake ya Mar-a-Lago estate - lakini halina uhusiano wowote na yeye kuwa...Read more »
Kupitia safu yetu ya mahusiano, leo nimekuletea makala maalum hasa kwa wanawake kutokana na malalamiko ya wanawake wengi kuwapoteza waume zao. Ki...Read more »
kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususani kwa...Read more »
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionHuenda ndege zikatengezwa bila madirisha katika siku za usoni.
Kampuni ya ndege ya Emirates imezindua nd...Read more »
Post a Comment
aprieztmkrdezign
218168578325095
Emoticon
Click to see the code! To insert emoticon you must added at least one space before the code.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.