0
Waziri wa fedha Henry RotichHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionWaziri wa fedha Henry Rotich
Wizara ya fedha nchini imekiri kwa serikali inakumbwa na changamoto kubwa za kifedha na haiwezi kabisa kutimiza mahitaji yake.
Ufadhili wa miradi muhimu ya serikali umeathiriwa zikiwemo serikali za kaunti ambazo bajeti zao, serikali itazipunguza kwa shilingi bilioni 15 na 17 (dola 147m na 167m).
Kutokana na ukosefu huo wa fedha mashirika ya serikali yametakiwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kutumia fedha zilizopo kwa njia inayostahili.
"Kila shirika ni lazima lijizatiti. Tumebuni njia ya kupunguza matumizi. Tunapunguza matumizi kwa kila sekta ili kwenda sambamba na fedha zetu," alisema waziri wa fedha Henry Rotich.
Amesema kuwa hali hii imetokana na kushindwa kwa halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya KRA kushindwa kutimiza malengo yake yote ya kukusanya ushuru na kipindi kirefu cha shughuli za uchaguzi.
"Tumeongea na KRA Jinsi tunaweza kukabiliana na hilo kupitia ukusanyaji wa kodi ya ndani na ya nje," Rotich aliiambia Kamati ya ya seneti.

Kenya yakumbwa na upungufu wa fedha

Bilioni 17
Upungufu kwa bajeti za kaunti
Bilioni 70
upungufu katika makadirio ya serikali ya mwaka 2017/2018
  • Trilioni 4.55 Deni la Kenya kufikia Desemba mwaka 2017
  • Bilioni 134 Zilizotolewa kwa serikali za kaunti
Kulingana na Rotich serikali inakabiliwa na upungufu wa ukusanyaji ushuru wa bilioni 70 kwenye makadirio ya serikali ya mwaka 2017/2018.
Kutokana hilo, kuna uwezekano kuwa wakenya watakumbwa na nyakati ngumu kwa sababu serikali itaendelea kukopa ndani ikishindana na watu, hali ambayo itachangia biashara ndogo kuwa na ugumu wa kupata mikopo kutoka kwa benki.
Hadi Desemba mwaka 2017 deni la Kenya lilikuwa shilingi trilioni 4.55, deni ambalo limesababisha nchi kutenga asilimia 54 ya pato lake kulipa madeni.
Maseneta walitaka kujua ni kwa nini serikali za kaunti hazijapokea fedha kwa miezi minne licha ya seneti kuidhinisha kutolewa kwa fedha hizo.
Alijibu na kusema kuwa ni shilingi bilioni 134 tu zimetolewa kwa serikali za kaunti kinyume na fedha zilizokuwa zikihitajika dola bilioni 302.

Post a Comment

 
Top