0
Image may contain: 1 person, smiling, standing
Hasani Makwendo (kushoto) akipokea vifaa vya michezo leo marchi 10 kutoka kwa mkuu wa wialaya ya Liwale Bi Sarah Chiwamba leo katika shule ya msingi Mbuli 
Image may contain: 2 people, people standing
MKuu wa wilaya ya Liwale Bi Sarah Chiwamba leo akabidhi vifaa vya michezo vilivyotelewa na Mashujaa fm 89.5 kwa timu tatu ambazo ni Mbuli fc,Nyela fc na Nyuki fc ambazo zilizopo katika kijiji Mbuli kata ya Kichonda wilayani Liwale.
Baada ya kukabidhi vifaa hivyo Abdeham Mtihania na Hasani Makwendo ambaye ni diwani wa kata ya Kchonda wametoa shukrani za dhati kwa Mashujaa fm 89.5 pamoja na mkuu wa wilaya ya Liwale kwa kuwawezesha kuwapatia vifaa hivyo vya michezo.

Wananchi wa wilayani Liwale mkoani Lindi wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na wametakiwa kuiunga mkono  serikali iliyopo madarakani ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe DK John Pombe Magufuli kwa lengo la kuwatumikia wananchi wake.

Wito huo ameutoa  mkuu wa wilaya ya Liwale mhe Sarah Chiwamba leo kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu tatu zilizopo katika kijiji cha Mbuli kata ya Kichonda  wilayani Liwale.

Mkuu wa wilaya amewasisitizi wananchi wawe na utamaduni wa kujiwekea akiba ya kutunza mazao ya chakula na kupunguza kufanya sherehe mbalimbali zisizo na tija ili kuepuka kutumia chakula kingi kwenye sherehe ambazo hazina tija.


Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mbuli kata ya kichonda wilayani liwale mkoani nao walipaza sauti zao huku wakiwataka wananchi wenzao kutii sheria zilizowekwa na kufanya kazi kwa bidii ilikuondokana na matatiao yasiyokuwa ya lazima.



Post a Comment

 
Top