Mmea wa muhindi uliyoshambuliwa na wadudu (picha na Liwale blog)
Wakulima wilayani Liwale mkoani Lindi wamewataka maafisa ugani kuwatembelea wakulima ili kuweza kutatua changamoto za wakulima wanazokumbana nazo ili kuongeza uzaishaji.
Wakulima hao waliyasema hayo nyakati tofauti tofauti wakati wakizungumza na mwandishi wetu na ndipo walivyobainisha kuwa wadudu aina ya funza wanavyoshambulia mazao na wakulima hao kukosa ufumbuzi juu ya kuwahangamiza wadudu hao.
Wadudu hao aina ya funza ambao hushambulia sana mimea ya mahindi,mpunga na aina za mbogamboga huku baadhi ya wakulima walisema kuwa mpaka sasa hawafahamu jinsi ya kuwahangamiza wadudu hao na wameiomba serikali iwasaidie kuwahangamiza wadudu hao wanaoshambulia mazao.
Salumu kiputi ambaye ni mkulima wa kilimo cha kiangazi na masika alisema kuwa tatizo la wadudu limemwathi sana katika mavuno yake huku akieleza kuwa aliweza kutumia dawa mbalimbali lakini na amewaomba maafisa ugani kwenda kuwatembelea na kuangalia wadudu wanaoathiri ni wa aina gani na wanatibiwa kwa dawa gani.
Salima Himbu ni mkulima wa kilimo cha mpunga alisema kuwa wadudu hao kwenye zao la mpunga hushambulia majani mara tu mpunga ukiota pamoja na kushambulia kwenye mizizi na aliomba serikali kuweza kuwasaidia ili kuweza kudhibiti kwa wadudu hao wanaombulia mazao yao.
Jacobo Mkongongonole mkazi wa kijiji cha Mungurumo wilayani Liwale ni mkulima wa bustani alisema kuwa zipi changamoto nyingi wanazokumbana naazo wakulima kama maradhi yapo ya aina nyingi lakini ugonjwa unaowatesa wakulima wengi ni kanitangaze ni jamii fulani ya funza ugonjwa ambao wakulima wengi hawajui watumie dawa ya aina gani ili kuweza kuudhibiti.
Mkongongonole alitoa rai kwa maafisa ugani wawe na ushirikiano wa kutosha na wakulima ili kuwapa uelewa kuhusiana na magonjwa haya kwakuwa wakulima wapo kanda mbalimbali ikiwa wengine vijini hivyo hawana uelewa wa kutosha juu ya kukabiliana na ugonjwa aina ya funza wanaoshambulia mazao.
Pia aliongeza kusema kuwa wakulima wanatakiwa wawe tayari kuipokea elimu itakayotolewa na maafisa ugani ili kuweza kupata mbinu mbalimbali za kudhibiti magonjwa yanayoshambulia mazao kwakuwa wakulima wengi hawafikiwi na vipeperushi pamoja na majalida yanayoelezea masuala ya kilimo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisa kilimo wilaya ya Liwale,Mustapha Magembe inaeleza kuwa Halmashauri inafahamu kuwepo kwa wadudu hao na maafisa ugani wote katika maeneo yao wamekuwa wakiwaelekeza wakulima namna ya kukabiliana na wadudu na ni vema wakulima wakawasiliana na maafisa ugani wao katika maeneo yao haraka ili wapate maelekezo.
Post a Comment