Chelsea watampa Eden Hazard ofa ya karibu pauni 300,000 kwa wiki wanapojaribu kuzuia vilabu vinavyommezea mate mchezaji huyo raia wa Ubelgiji ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2020. (Mail)
Barcelona wanamuangalia mlinzi wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld, 28 ambaye sehemu ya mkataba wake inasema kuwa anaweza kuruhusiwa kuondoka kwa pauni milioni 25 msimu wa joto mwaka 2019 kama hajakubaliana na mkataba mpya. (Independent)
Paris St-Germain watamuachilia mshambulizi raia wa Ufaransa Kylian Mbappe, 19, kwa Barcelona, kumbadilisha na Philippe Coutinho. Wanajaribu kumpendekeza mshambulizi raia wa Brazil Neymar ambaye anasema hapendezwi na Mbappe lakini ni rafiki wa Coutinho, 25. (El Pais)
Borussia Dortmund wametoa ofa kuwakabili Bayern Munich katika kumsaini mshambulizi wa Bordeaux Malcom. MBrazil huyo wa miaka 21 amekuwa akilengwa na Tottenham. (Sun)
Dortmund wanahofu kuwa huenda wakakosa kumsaini mshambulizi wa mkopo wa Chelsea Michy Batshuayi kwa mkataba wa kudumu msimu huu kwa kuwa mchezaji huyo amevutia vilabu vingine kutokana na mchezo wake mzuri. (Kicker, via London Evening Standard)
Chelsea na Manchester United wote watajaribu kumsaini mshambulizi wa Poland, Robert Lewandowski ikiwa mchezaji huyo wa miaka 29 ataishawishi Bayern Munich kumuachilia kutoka mkataba wake unaokamilika mwaka 2021. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Southampton Harrison Reed anasema hataki kurudi katika benchi baada ya kufanya mazoezi wiki yote na kukosa kushirikishwa kwenye mechi. Mchezaji huyo yuko kwa mkopo huko Norwich. (Daily Echo)
Tottenham wanatarajiwa kucheza mechi tatu au nne za msimu ujao nje ya uwanja wa White Hart Lane wakati uwanja huo unafanyiwa ukarabati. (Independent)
Mshambulizi wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anasema kuwa ameshinda vitu vingi vizuri na sasa hana ndoto nyingine.(Marca)
Kiungo wa kati wa Manchester United Nemanja Matic anasema anataka klabu yake ya zamanai Chelsea kuwapita Tottenham na kumaliza katika nafasi ya nne katika Premier League. (London Evening Standard)
Mshambulizi wa Manchester United Romelu Lukaku anaamini ahitaji kupewa heshima zaidi. Mchezaji huyo raia wa Ubelgiji wa umri wa miaka 24 amefunga mabao 98 katika mechi 213 amecheza katika Premier League. (Sky Sports)
Post a Comment