Taarifa zilizotufikia hapa asubuhi hii ya leo ya February 2, 2018 ni kwamba Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia alfajiri ya leo.
Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam takriban mwezi mmoja uliopita.
Mke wa Kingunge Peras Ngombalemwiru alifariki dunia mwanzoni mwa mwezi January kutokana na ugonjwa wa kupooza kipindi ambacho Mzee Kingunge alikuwa tayari anapatiwa matibabu ya majeraha hayo.

Post a Comment