0
Tokeo la picha la ajinyonga
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Chande Nasoro Ngaluya mkazi wa kata ya nangando wilayani liwale mkoani lindi amefariki dunia kwa kujinyonga na kamba.

Chande Nasoro Ngaluya ni mkulima mwenye umri wa miaka (40) ambaye alikuwa anafanya shughuli zake za kilimo huko katika kijiji cha Lilombe kata ya lilombe wilayani liwale,huku kukielezwa sababu hasa za kujinyonga kwake ni kile kinachodaiwa kuwa na mapungufu ya akili.

Kwa mujibu wa Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni watu walio karibu na marehemu kama rafiki yake Twahili Mmulila na Chande ally ngaluya walisema kuwa marehemu kwa mara ya kwanza anasakikika kuwa na tatizo la akili lilomwazia kijijini kwao Lilombe.

Mmulila na Chande ally ngaluya walisema kuwa leo asubuhi febuari 6 kabla ya kijana huyo hajachukua hatua ya kujinyonga walitarajia kukaa kikao ili kuweza kumpeleka kesho febuari 7 kwenye tiba. 

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Liwale,Dk Kassanga Evaristo Benito alieleza kuhusiana na matokeo ya uchunguzi wa mwili wa marehemu na amethibitisha kutokea kwa kifo hicho kwa kujinyonga kwa kamba.

Dk Kassanga ametoa wito kwa jamii kuwa wanapohisi mtu ana dalili ya tatizo la afya ya akili wanatakiwa kumpeleka hospitali mapema ili kumfanyia vipimo na kumpa matibabu mapema.


Post a Comment

 
Top