Na Agness Francis, Blogu ya jamii
KLABU ya Yanga ya Dar es Salaam imesaini mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya Macron kutoka Itali kwa lengo la kutengenezewa jezi za kimataifa zenye thamani ya Sh.bilioni 2.
Makubaliano ya utiaji saini mkataba huo umefanywa leo Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Yanga Boniphace Mkwasa na Mkurugenzi Kampuni ya Macron Tanzania Suleiman Karimu.
Akizungumza baada kusaini mkataba huo, Mkwasa pia amesema kwa wale wanaouza jezi mitaani kwa manufaa yao binafsi ambayo hayanufaishi klabu yao waache mara moja.
"Kwa wataoendelea na biashara hiyo watachukuliwa hatua,"amesema Mkwasa.
Kwa upande wa Mkurugenzi kampuni ya Macron Tanzania, Suleiman Karimu ameishukuru klabu ya Yanga kwani makubaliano hayo yataleta mapinduzi ya mpira wa miguu hapa nchini.
Post a Comment