Gari moja lililokuwa linaendeshwa kwa kasi katika jimbo la California liliruka na kuingia ndani ya ghorofa ya juu kwenye jumba moja baada ya kugonga uzio wa kutenganisha barabara, taarifa zinasema.
Ajali hiyo, ambapo sehemu moja ya gari ilibaki ikining'inia nje ya jengo hilo, ilitokea mapema Jumapili asubuhi.
Watu wawili waliokuwa ndani ya gari hilo walinusurika na majeraha madogo, kwa mujibu wa polisi.
Polisi wameambia wanahabari kwamba dereva wa gari hilo anadaiwa kutumia dawa na alikuwa ametembelea hospitali moja.
- California yaidhinisha matumizi zaidi ya bangi
- Matumizi ya bangi sasa ni halali California
- Mwanamume achoma nyumba akiua buibui Marekani
- Kampuni ya bangi yaununua 'mji wa bangi' Marekani
Mmoja wa wawili hao alifanikiwa kujitoa kutoka kwenye gari hilo lakini huyo mwingine alikwama kwa zaidi ya saa moja hadi maafisa wa uokoaji walipofika.
Ajali hiyo pia ilisababisha kuzuka kwa moto mdogo ambayo wazimamoto walifanikiwa kuuzima.
Wazimamoto walipakia picha za kisa hicho na walikuwa wanawapata watu yaliyokuwa yakijiri siku yote..
Kisa hicho kilitokea Santa Ana, maili 35 (56km) kusini mwa Los Angeles.
Post a Comment