Mwanamume mmoja ametoroka nchini Burundi baada ya kuwapa adhabu ya kikatili watoto wake wawili ambao inadaiwa aliwapata wakiiba mahindi kwenye shamba lake.
Mwanaume huyo aliwazika ardhini wanawe wawili hadi sehemu ya vifua kabla ya kuwachapa viboko.
Walibahatika kuokolewa na mpita njia ambaye alikuwa jirani yao .
Kulingana na taarifa ya mwandishi wa BBC Prime Ndikumagenge kutoka Bujumbura.
Tukio hilo la ajabu lilitokea katika kijiji cha Bubanza, mkoa wa kaskazini magharibi mwa mji mkuu Bujumbura Jumapili jioni.
- Tanzania kupiga vita ukatili wa kijinsia
- Ukatili wa kijinsia bado ni kikwazo Tanzania
- 'Muathiriwa wa ugonjwa wa ukimwi adai kubakwa na watu watatu Kenya'
- Tanzania yasimamisha huduma za vituo 40 vya afya
Taarifa zinasema watoto hao wenye umri kati ya miaka 8 na 10 walikamatwa wakiwa wanaiba katika shamba la mahindi.
Mmiliki wa shamba hilo aliamua kuchimba mashimo mawili na kumzika kila mmoja wao hadi usawa wa vifua vyao na kuanza kuwatandika viboko.
Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa hawajui ni nini kingetokea kwa watoto hao kama jirani yao asingepita.
Mwanaume huyo kisha alitoroka na watoto hao wakaokolewa.
Polisi wanasema bado wanamsaka mwanaume huyo kwa ajili ya kumfikisha mbele ya sheria.
Si mara ya kwanza kwa tukio la aina hii la kikatili dhidi ya watoto kufanyika nchini Burundi.
Watoto wawili walikatwa mikono yao ya kushoto katika jimbo la kati la Gitega mwezi Novemba mwaka jana baada ya kupatikana wakiiba mahindi.
Post a Comment