0


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

VINARA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC leo wanatarajiwa kuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza Saa 1:00 usiku na utaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Azam TV kupitia chaneli yake ya Azam Sports 2. 

Kocha Mkuu wa Wekundu hao wa Msimbazi, Joseph Marius Omog anataka kuutumia mchezo huo kuwachangamsha wachezaji wake, kufuatia Ligi Kuu kusimama kupisha michuano ya CECAFA Challenge inayoendelea nchini Kenya.

Mchezo huo unakuja baada ya Simba SC kufanya mazoezi kwa takribani siku nne kuanzia Jumatatu, kufuatia mapumziko mafupi ya wiki moja.

Omog anaamini timu hiyo ya Daraja la Kwanza, KMC itawapa kipimo kizuri wachezaji wake baada ya mapumziko hayo mafupi.

Simba SC inaongoza Ligi Kuu baada ya mechi 11, ikiwa imejikusanyia pointi 23 sawa na Azam FC wakiwazidi kwa pointi mbili mabingwa watetezi, Yanga SC.

Post a Comment

 
Top