0
 Moja ya ghali la kukusanyia korosho wilayani Liwale zikiwa zimejaa kwenye ghala kwa kukosa usafiri pamoja na uhaba wa magunia hali inayopelekea kusota kwa mizigo ghalani.(Picha na Liwale Blog)
Mbunge wa Jimbo la Liwale,Mhe.Zuberi Kuchauka alipofanya ziada kwenye magahala ya kukusanyia korosho leo desemba 4 kwenye vyamaba mbalimbali.








Vyama vya ushirika wilayani Liwale vyalalamikia uhaba wa magari ya usafirishaji pamoja na uhaba wa magunia hali inayopelekeaa mizigo kurundikana maghalani.

Wakizungumza na mbunge wa jimbo la Liwale,mhe.Zuberi Kuchauka kwa nyakati tofauti tofauti leo alipotemblea maghalani baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika wamesema kuwa kutokana na uhaba huo inapelekea korosho kuendelea kurundikana ghalani na kuchelewa kuzifikisha kwenye ghala kuu kwa ajili ya mnada.

Ziara hiyo ya mbunge mh. Kuchauka ameifanya mara baada ya kupokea malalamiko kwa wakulima kuchelewa kupokea fedha zao huku viongozi wakisema tatizo korosho nyingi zimebaki kwenye maghala kwa kukosa magari ya usafirishaji pamoja na tatizo la maguni.

Kuchauka amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kuandaa orodha ya wakulima ambao korosho zao zitakazo safirishwa kwa ajili ya kusubiria mnada husika ili kupunguza malalamiko .

Baadhi ya viongozi na wakulima hawana elimu ya ubora wa korosho na juu ya mfumo kama mwandishi wetu alipozungumza na makamu mwenyekiti wa chama cha ushirika

Post a Comment

 
Top