Kocha mkuu wa Chelsea FC Antonio Conte baada ya kupigwa faini ya paundi 8000/- baada ya kukwaruzana na waamuzi katika mechi yao dhidi ya Swanswea nakutolewa nje ya uwanja dakika ya 42, amesema hatamnunulia mkewe zawadi ya kumbukizi ya kuzaliwa itakayoadhimishwa tarehe 4 December.
Conte aligombana na waamuzi akilazimisha wakubali pigo la kona timu hizo zikiwa bado 0-0 hali iliyopelekea kutolewa uwanjani na kumalizia mechi akiwa chumba cha kubadilishia nguo.
” lilikuwa ni kosa na nimejifunza wakati mwingine nitawaambia wachezaji wangu ndio waongee na mwamuzi lakini ni dhahiri tulinyimwa kona” alisema kocha huyo baada ya kukubali kosa lake.
Mke wa kocha huyo Elisabetta Conte alikuwa uwanjani na binti yao akishuhudia mumewe akitolewa nje ya uwanja baada ya makosa hayo na mwamuzi Neil Swarbrick kigezo ambacho Conte anakitumia mwanamke huyo amuelewe kwamba hawezi kumnunulia zawadi ya siku yake ya kuzaliwa ili kufidia gharama za adhabu hizo.
‘ najua atakuwa amekasirika lakini siwezi kutumia fedha za klabu kwa kosa langu hivyo familia nzima lazima iungane na mimi katika hili ” alisema Conte huku akicheka.
Wadukuzi wa mambo wamekuwa wakilichukulia jambo hili kama mzaha wa Conte katika kujiweka sawa kisaikolojia baada ya kufanya kosa la kuwafokea waamuzi na wanaamini atamnunulia zawadi bi Elisabetta.
Post a Comment