Kisima Cha Maji Kilichochimbwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR)katika Kijiji cha Kasanda ambacho kitawanufaisha Wananchi wa Maeneo hayo na Wakimbizi waishio katika Kambi ya Mtendeli Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.
Moja wapo ya bomba la maji yaliyosambazwa ndani ya Kambi ya Wakimbizi Mtendeli kutoka katika mojawapo ya Visima Vilivyochimbwa katika Vijiji Jirani na eneo la Kambi.
Wahandisi wa Maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) na Shirika la TCRS wakikagua chumba chenye mashine ya kuchuja na kusafisha maji yanayotoka katika kisima kilichochimbwa kwa ajili ya matumizi ya Wakimbizi waishio katika Kambi ya Mtendeli Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma.
Mhandisi wa Maji kutoka shirika la TCRS Linalofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),Emmanuel Busanga akitoa maelezo juu ya mahitaji ya maji katika kambi ya Mtendeli iliyopo Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma
Muhandisi wa Maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),Mukiza Florinus akitoa maelezo kwa Mwandishi wa habari wa Gazeti la The Guardian ,Getrude Mbago ambaye ni sehemu ya ujumbe wa waandishi watano waliotembelea kambi za wakimbizi
Post a Comment