0

Mwakilishi mkazi wa Shirika la The Desk and  Chair Foundation  Sbtain P.L Meghjee  (shati la drafti) akikabidhi kisima katika moja ya maeneo ambayo wametoa huduma hiyo hapa nchini .

Na David John Mwanza .

TAASISI ya kijamii ya The Desk and Chair Foundation ya jijini Mwanza imetoa rai kwa Serikali kuwa na mawasiliano ya karibu ili kujuwa changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo watanzania hususani wenye uhitaji maalum. 

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Ofisini kwake jijini hapa Mwakilishi mkazi wa Taasisi hiyo hapa nchini yenye Makao yake Makuu nchini Uingereza Sibtain P.L Maghjee amesema kuwa taasisi yake inashughulika na matatizo ya watu hususani walemavu na hata jamii kwa ujumla. 

Amesema kuwa changamoto kubwa wanayokutana nayo ni kukosekana kwa mawasiliano ya karibu kutoka Serikali ili kupata takwimu za watu au jamii yenye uhitaji. " Taasisi yetu imekuwa ikifanya kazi nyingi katika jamii ikiwamo kuchimba Visima pamoja na kusaidia Ambulence kwa ajili ya wagonjwa katika vituo vya afya. mbalimbali hapa nchini na zaidi vijijini "amesema Meghjee 

Akizungumzia zaidi taasisi hiyo amesema mbali na huduma hizo lakini pia wamekuwa wakitoa mafunzo mbalimbali ya ufundi, wa aina mbalimbali kwa vijana ambapo mwisho wa siku wanajiajiri wenyewe. Amesema kuwa wao kama taasisi pia wanatengeneza Ambulence kwa kutumia mafundi hao ambao wanafundishwa kupitia Kalakana yao iliyopo Greenview eneo la Ghana jijini hapa. 

Pia akizungumzia misaada wanayoitoa amewataka wananchi kutunza miundombinu hiyo hususani visima ambavyo wanakabidhiwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini na kuvithamini. " Unajuwa Ndugu mwandishi lazima watu wajenge nidhamu ya kutunza na kuthamini vitu ambavyo wanapewa kwani kufanya hivyo kunawapa moyo hata watu wanaotoa. "amesema. 

Amesema licha ya uchimbaji wa visima hivyo lakini pia taasisi imekuwa ikifanya mambo mbalimbali tangu kuazishwa kwaks mwaka 1979 hapa nchini na wametengeneza basikeli 30 kwa ajili ya walemavu ambazo zitakabidhiwa hivi karibuni. 

Post a Comment

 
Top