GETTY IMAGES
Baada ya mataifa 32 kufanikiwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Urusi, droo ya kupanga makundi ya timu hizo itafanyika Ijumaa ya Desemba 1 mjini Moscow.
Kuelekea zoezi hilo baadhi ya Timu ambazo zimepangwa chungu kimoja ni chungu cha kwanza ambacho kina timu mwenyeji Urusi, Ujerumani, Brazil, Ureno, Ajentina, Ubelgiji, Poland na Ufaransa.
- Mambo muhimu kuhusu nchi ambazo tayari zimefuzu Kombe la Dunia 2018
- Taifa la watu 335,000 lafuzu Kombe la Dunia
Afrika inawakilishwa na Misri, Nigeria, Morocco, Tunisia na Senegal.
Na kuelekea fainali hizo FIFA wamesema mpaka sasa kuna maombi milioni 3.5 ya tiketi na walioomba wengi wao ni wenyeji Urusi.
Vyungu vimepangwa vipi?
| Vyungu Kombe la Dunia | |||
|---|---|---|---|
| Chungu 1 | Chungu 2 | Chungu 3 | Chungu 4 |
| Urusi (wenyeji) | Uhispania (8) | Denmark (19) | Serbia (38) |
| Ujerumani (1) | Peru (10) | Iceland (21) | Nigeria (41) |
| Brazil (2) | Uswizi (11) | Costa Rica (22) | Australia (43) |
| Ureno (3) | England (12) | Sweden (25) | Japan (44) |
| Argentina (4) | Colombia (13) | Tunisia (28) | Morocco (48) |
| Ubelgiji (5) | Mexico (16) | Misri (30) | Panama (49) |
| Poland (6) | Uruguay (17) | Senegal (32) | Korea Kusini (62) |
| Ufaransa (7) | Croatia (18) | Iran (34) | Saudi Arabia (63) |

Post a Comment