0
Mugabe akimsalimia mkuu wa jeshi la wanahewa Perence ShiriMugabe akimsalimia mkuu wa jeshi la wanahewa Perence Shiri

  1. MugabeRais Robert Mugabe ameashiria kwamba ataendelea kuliongoza taifa hilo
  2. Awali, chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF kilikuwa kimemvua uongozi wa chama Robert Mugabe
  3. Zanu-PF imemteua aliyekuwa makamu wa rais Emmerson Mnangagwa ambaye alifutwa wiki mbili zilizopita kama kiongozi wake.
  4. Jeshi la Zimbabwe lilichukua hatamu za kiserikali na kumweka Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani
  5. Maelfu ya raia wa Zimbabwe Jumamosi walijitokeza barabarani mjini Harare katika jitihada za kuongeza shinikizo za kumtaka rais Mugabe ajiuzulu

Mugabe amaliza hotuba bila kujiuzulu

Wengi walitarajia kwamba Rais Robert Mugabe angetumia hotuba yake ya moja kwa moja kwenye runinga kujiuzulu, hasa baada ya kuvuliwa uongozi wa chama cha Zanu-PF.
Lakini hilo halijafanyika.
Badala yake amesema ni yeye atakayeongoza mkutano mkuu wa chama hicho wiki chache zijazo.
Amewahimiza raia wa Zimbabwe kuvumiliana na kusameheana.

Post a Comment

 
Top