0
                                   
      
Matukio ya ukatili na unyanaysaji wa wanawake na watoto wadogo yaekua yakiongezeka siku hadi siku katika jamii yetu.Licha ya kuwepo kwa ukatili wa kimwili,Kingono,Kiakili,

Kiuchumi n.k.ukatili wa kingono ndio umekua ukiongezeka kila siku hasa ubakaji kwa watoto wadogo.Ni jambo la kusikitisha ni kwamba ukatili huo mara nyingi umebainika kufanywa na watu a karibu ndani ya familia.

shirika la hakielimu limebaini kuwepo na mapungufu makubwa kwa jamii kutochukua hatua katika kuwalinda watoto dhidi ya ukatili na unyanyasaji.hata hivyo kumekua na matukio mengi ya ukatilia na unyanyasaji  katika jamii yetu ambayo yamekua hayaripotiwi katika vyombo vya sheria.sababu kubwa ni uchache wa vyombo vya habari.

Hali hiyo imewafanya shirika la hakielimu kuandaa mpango kazi wa miaka mitano katika shughuli moja wapo ni kutokomeza Unyanyasaji na Ukatili dhidi ya wanawake na watoto.Kuanzia tarehe 29/06/-01/07/2017 shirika la hakielimu liliendesha mafunzo kwa marafiki wa Elimu 17 toka kanda ya kusini toka wilaya ya Kilwa,Masasi,Tunduru, na Mkuranga kuudhuria mafunzo ya kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto,Pia marafiki hao wamepata mafunzo ya uhandishi wa habari za kijamii kwa kujitolea(CIVs).

Kukamilisha kwa mafunzo haya itawezesha marafiki kuweza kufichua matukio mengi ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya wanawake na watoto yanaripotiwa(Kufichuliwa).Na jamii pia kupewa elimu juu ya umuhimu wa  kuwalinda watoto wao.sasa nifursa kwa wananchi wa wilaya za kanda ya kusini tajwa hapo juu kuona umuhimu wa waandishi hawa kwa vile wanatokea katika ngazi za kijamii ni muhimu kuona wanawatumia vema waandishi hao katika kutokomeza unyanyansaji  wa kijinsia na ukatili kwa wanwake na watoto.Pia kupunguza uchache wa waandishi wa habari waliopo kanda ya Kusini .

Rafiki wa Elimu Kilwa -0685375660

Post a Comment

 
Top