0
Cristiano RonaldoHaki miliki ya pichaEPA
Cristiano Ronaldo ameshinda taji la shirikisho la soka FIFA la mchezaji bora wa kiume wa kandada mwaka huu kwa mara ya pili mtawalia.
Mchezaji huyo kutoka Ureno, amefunga mabao 44 katika mechi 48 alizoshiriki katika mwaka, kuiwakilisha nchi yake pamoja na timu anayoichezea ya Real Madrid aliochangia kufanikisha ushindi wake katika mataji ya ligi ya Uhispania La Liga na ligi ya mabingwa Ulaya - Champions League.
Lieke MartensHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLieke Martens
Alipokea tuzo yake mjini London na aliwashukuru mashabiki wake wa Real Madrid, wachezaji wenzake, kocha na rais wake.
Tuzo hiyo kwa mchezaji bora mwanamke aliinyakuwa mchezaji wa Uholanzi Lieke Martens, anayeichezea Barcelona.
Aliwahi pia kuichezea timu ya taifa ya Uholanzi iliposhinda mashindano ya Euro 2017.

Post a Comment

 
Top