0

Mwalimu mkuu shule ya msingi Kambarage,Hashimu Libena (kushoto) na Katibu tawala wa Halmshauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi,mhe.Mbwana Kambangwa  (aliyesimama)  akizungumza na wazazi pamoja na walezi leo septemba 4 katika shule ya msingi Kambarage iliypo kata ya Nangando wilayani Liwale.
Wazazi na walezi walioudhulia kwenye kikao leo katika shule ya msingi Kambarage wilayani Liwale .
Wazazi na walezi walioudhulia kwenye kikao leo katika shule ya msingi Kambarage wilayani Liwale 
Katibu tawala wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale akikabidhi chakula kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la saba wanaotarajia kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi.

Katibu tawala wa Halmshauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi,mhe. Mbwana Kambangwa amewataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa walimu ili kuhakikisha wanapiga hatua ya maendeleo katika kutoa elimu bora kwa watoto wao.

Ameyasema hayo leo septemba 4 akikabidhi chakula kwa ajili ya wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani wa darasa la saba katika shule ya msingi Kambarage iliyopo kata ya Nangando wilayani Liwale.

Aidha mhe. Kambangwa amesema kuwa ametoa msaada huo wa chakula kwa kuwaunga mkono kutokana na jitihada  zinazofanywa na walimu kwa kushirikiana na wazazi shuleni hapo ili kuhakikisha wanapiga hatua kubwa ya maendeleo katika kutoa elimu bora kwa watoto wao pia amewasisitiza wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mema na kuwajengea misingi imara ya maisha yao.

Kwa upande wa wazazi Bi Nuru Mpoto na Bw. Ubaya Mwingira  wakingumza kwa niaba ya wazazi wengine wamemshukuru katibu tawala kwa msaada alioutoa kwani umeonyesha kuiunga mkono  jamii anayoitumikia na wamewaomba wazazi kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya watoto wao wawapo shuleni.

Pia Mwalimu mkuu  wa shule hiyo Hashimu Libena amemwakikishia katibu tawala wataendelea kudumisha ushirikiano uliopo pia  ufaulu wa wanafunzi utaongezeka shuleni hapo.

Post a Comment

 
Top