Wanajeshi wa Ubelgiji wanamtafuta rubani wa helikopta ya jeshi ambaye alianguka kutoka kwa ndege hiyo wakati wa maonesho ya ndege za kivita.
Wanajeshi watatu waliruka kutoka kwa helikopta hiyo aina ya Agusta A-109 wakiwa na parachuti, lakini rubani huyo na msaidizi wake hawakuwa na parachuti, vyombo vya habari Ubelgiji vimeripoti.
Taarifa zinasema rubani msaidizi aliwasaidia wanajeshi hao watatu kuruka nje, lakini aliporudi kutazama kiti cha rubani akashangaa kupata rubani hayupo.
Alichukua usukani na kuanza kuiongoza ndege.
Maonesho hayo yalikuwa yakifanyika katika eneo la Amay, karibu na mji wa Liège.
Rubani huyo alianguka mita mia kadha kutoka angani.
Sababu ya rubani huyo kuanguka bado haijulikani.
Post a Comment