Wanafunzi saba wamefariki na makumi wengine wakijeruhiwa baada ya moto kuchoma bweni la shule ya Moi Girls mjini Nairobi.
Waziri wa elimu Fred Matiang'i amesema kuwa wanafunzi wengine 10 walijeruhiwa na wamelazwa hospitalini.
Wawili kati ya 10 wako katika hali mbaya ,kulingana na madaktari huku wengine wanane wakiwa hawako katika hali mbaya.
Takriban wanafunzi 10 wamerodheshwa kuwa hawajulikani waliko kulingana na kitengo cha habari cha maafisa wa msalaba mwekundu katika shule hiyo.
Matiang'i amesema kuwa shule hiyo imefungwa kwa wiki mbili huku uchunguzi ukianzishwa kuhusiana na sababu ya moto huo.
Waziri huyo hatahivyo amesema kuwa wanafunzi wa kidato cha nne wataendelea na masomo yao ifikiapo siku ya Ijumaa na watasaidiwa kuendelea na masomo yao wakati ambapo wanajianda kufanya mtihani wa kidato cha nne wa KCSE.
Amesema kuwa kundi la wataalam wa upasuaji ikiwemo madaktari wako katika shule hiyo kubaini chanzo cha moto huo.
Amesema kuwa mkuu wa shule hiyo amewataka wazazi kuwachukua wanawao.
Bwana Matiang'i aliandamana na gavana wa Nairobi Mike Sonko.
Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini humo mwanafunzi mmoja wa kidato cha kwanza ambaye alikuwa miongoni mwa wale waliotibiwa baada ya kisa hicho alisema kuwa moto huo ulianza mwendo wa saa saba usiku.
Alisema kuwa bweni lililochomeka lilikuwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza na kwamba kulikuwa na makelele ya wanafunzi waliojaribu kujinusuru mbalii na mkanyagano huku wasichana wakijaribu kutoka ndani ya bweni hilo.
Post a Comment