0


TAARIFA KWA UMMA

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuwataarifu Wadau wa Elimu na Umma kwa ujumla kwamba mafunzo ya Wauguzi Wasaidizi (Nurse Assistants) na Wahudumu wa Afya (Medical Attendants) si miongoni mwa mafunzo yanayosimamiwa na kutambuliwa na Baraza, na kwamba chuo chochote kinachotoa na kuendesha mafunzo hayo kinakiuka Kanuni za Usajili pamoja na Kanuni za Ithibati za Baraza za mwaka 2001.

Kwa tangazo hili Baraza linawatahadharisha wananchi kwa ujumla kutojiunga na mafunzo yaliyotajwa hapo juu kwa kuwa tuzo zinazotolewa baada ya kuhitimu mafunzo hayo pia hazitambuliwi.

Aidha Baraza linaendelea kufuatilia na kuvibaini vyuo vyote vinavyotoa mafunzo hayo kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki. Kituo au chuo chochote kitakachokutwa kinatoa mafunzo ya aina hiyo, wahusika watakabidhiwa kwenye vyombo vya Sheria kwa udanganyifu na kutoa mafunzo yasiyotambuliwa na Baraza na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.

Imetolewa na:
Kaimu Katibu Mtendaji,
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
18/09/2017

Post a Comment

 
Top